Waziri Jafo amuondoa kwenye nafasi yake Meneja wa TARURA jijini Arusha kwa kushindwa kuita Wananchi kushuhudia ufunguzi wa barabara

ERB sio watetezi wa Engineers,kazi yao sikuhizi ni kubuni vyanzo vya mapato..mtu alipe annual fees bado atakiwa kurenew leseni kila Mara na kulipia..Hawashirikishi wadau ktk maamuzi wanayofanya!,na hawana Sera zakutetea Engineers!
 
F Fedha ni kodi ya Wananchi na siyo jukumu au hisani ya Rais,hivi kila Barabara,mradi,faraja,handaki,meli,treni,daraja nk lazima izunduliwe na Rais atajwe katoa fedha,zake?
 
Kama unajua unajua tu,hauhitaji kujieleza sana watu wenyewe wataona tu
Badala ya kumpongeza Meneja wa TARURA na timu yote iliyoshiriki Ujenzi wa hizo Barbara,anaambulia kutumbuliwa kwa suala ambalo ni nje ya majukumu yake,Meneja/Engineer kazi yake kualika Wananchi kushiriki uzinduzi wa miradi?

Tuache mihemko ya kujipendekeza,inawaumiza na kuwakatisha tamaa watumishi/wataalam huku mkijisifia kwa uzuri na ufanisi wa kazi walizosimamia under pressure and stress mnazowabebesha-Hatari ya kutumbuliwa hata kwa kufanya vizuri,mkubwa asipopata sifa hapo unatumbuliwa.
 
Jamaa anatengeneza mazingira ya kurudishwa barazani kwa kujifanya ana spirit ya utumbuzi kama mkuu
 
Kwahiyo wandengereko wote wewe unawajua?
Nitajie hata mndengereko mmoja tu aliye hata na diploma tu unayemjua anayejulikana .HUWEZI LINGANISHA MZARAMO NA MNDENGEREKO
 
Jafo namkubali ila sababu alizotoa kwa meneja wa TARURA ni za kijinga na kishamba kupindukia.
Jamaa eti ameificha barabara..machalii wa A town nao hawajaona ili wajae..

Hapo angemtumbua mwenyekiti ccm,katibu na mwenezi wake wa hapo Arusha.

Kisha onyo kwa Bashiru na Polepole.
 
Ignorance is the new normal in fact ignorance is the new excellence the less you know the more seemingly you gain ...by Mwalimu kashasha...Cheap popularity stunt by the minister...
 
Hela za miradi zijumuishe hela ya matangazo ya kuwaalika wananchi kwenda kwenye uzinduzi wa miradi mbalimbali, wakigoma, nguvu itumike kuhakikisha wanakwenda kuhudhuria.
Wataalamu washirikiane kwa ukaribu na ofisi ya mkuu wa wilaya ili kufanikisha hilo
 
Duh, kazi hizi ngumu sana, ingefaa huyu mtendaji wa TARURA afanye mawasiliano ya kutosha nini na nini atahitaji waziri kabla ya kufika site. Nadhani hakukuwa na mawasiliano mazuri kabla
Jukumu la kukusanya watu siku hizi ni la injinia?
 
na yule GEORGE Aliyekua anamuita we joji mtoe huyu tumtafutie huko kwingine sijui kwakwere sijui wapi NI NANI?
Usikute ndio wambeya wenyewe hao wnataka cheo cha jamaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…