Waziri Jafo amuondoa kwenye nafasi yake Meneja wa TARURA jijini Arusha kwa kushindwa kuita Wananchi kushuhudia ufunguzi wa barabara

Jafo kafeli sana, bila shaka jafo alikuwa na jina lake mfukoni , asisingizie kutokuwepo kwa wanainchi, soon tutaona kimada hapo Arusha Tarura.

Viongozi wetu hawaijui sheria, sheria yenyewe inawajua japo hawataki kuisikiliza
 
Waende kanda ya ziwa, ndiyo kuna makondoo mengi na mazuzu ya kumwaga.
Yaani kila nikiisikiliza hiyo video na malalamiko ya jafo nashindwa kumuelewa alipatwa na tatizo gani maana anaonekana kabisa ana jambo lingine na uyo jamaa, jafo kwa hilo umeniangusha sana
Yaani lijafo limeonesha upopoma wa hali ya juu, huwa anaonekana ni mtu smart kumbe nae ni garbage tu.
Sielewi jafo katelezaje maana kafanya jambo ambalo liko chini sana sana wakati haikuwa hulka yake na hataki hata kumsikiliza jamaa ajieleze kitu ambacho ni uonevu mkubwa sana na shida watumishi hawana mtetezi kabisa kwa sasa
 

Shura ya Maimamu Tanzania baada ya waraka wenu wa jana, mnasemaje sasa juu ya muislamu Seleimani Jafo? Mkinyimwa uongozi/mamlaka ni nongwa!!!.
 
Jafo ni aina ya vingozi wanaochumia tumbo. Sijawahi furahiaga kazi zake hata kidogo..
 
Kwani kazi ya Magufuli au serikali ya Tanzania.Yaani awamu hii ina ubinafsi sana hela ni za wananchi sio za Rais jamani tubalike
 
Nimedharau sana aisee..kama ni kweli!.kwa clip vipi?
 
Inaonyesha alitumwa kumuondoa, hata watu wange kuwepo angeuliza mbona taa haziwaki? Huyu Mhandisi alikuwa rafiki wa yule alie tumbuliwa last week. Kwa hiyo huu ni mwendelezo wa kufafia makombo. Tuta sikia mengi. Maana hawezi tuu kushuka kwenye gari na kuulizia watu badala ya kufanya ukaguzi wa kilicho mpeleka. Mbaya zaidi hata baada ya maamuzi yake ya kishabiki hakufanya ukaguzi.
Haya ni matumizi mabaya ya kodi za wananchi na rasilimali zetu.
 
Mimi nadhani ni Sawa tu,

Maana yake halisi ni Sawa na Baba kujenga nyumba ya pili Halafu asiimbie familia yake kuwa amejenga nyumba nyingine mahali, Halafu akaweka wapangaji wasijue hata familia yake
Barabara itapita wapi na wananchi wasiione hata utake uwaonyeshe kitu ambacho komepita kwenye maeneo yao.
Jafo aseme tu kuwa alikuwa anamuwinda kwa muda mrefu huyo engr ila alishindwa kumpata, akaamua kutafuta sababu zisizo na mashiko hata kidogo. SHAME
 
Jaffo badala ya kuwasifia wananchi waliolipa kodi zilizotumika kujengea barabara anataka wananchi waje wamsifu mtu anayelipwa kusimamia matumizi ya kodi za wananchi.
 
Hivi George ni nani ? Maana nilikua nasikia Jafo anasema George,George kila mara
 
Watu wengi tulimheshimu Jafo lakini kwa hili la jana, mh amejipaka matope yanayonuka.
Kuna harufu ya visasi kwenye maamuzi yake hayo.
Mungu amhurumie Jafo[emoji120]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…