mheshimiwamtemi
JF-Expert Member
- Oct 27, 2014
- 291
- 218
Tume ya mipango haikai tu na kuota kuwa tupange nini .hAWAINUI TU VICHWA HEWANI na kuja na mawazo toka angani kuwa tupange hivi!!Ndo umejifunza wapi hayo???
Hivi ulikuwa unajua kazi ya tume ya mipango?? Unajua pia kuwa saivi imeamishiwa wizara ya fedha??! Unajua wanafanyaga nini??!!
Huo ndo ubaya mtu anahukumiwa bila hata ya kusikilizwa so sad ukweli ni kuwa haikutakiwa ifike hatua hiyo sometimes viongozi wetu inabidi wawe humble na wajue namna gani kudeal na watu ukali na maamuzi magumu hayakufanyi kuwa kiongozi bora bali itakufanya kuwa adui ya wale unaowasimamiaHii ndio sababu ya kumtoa mtu kazini.......this is Insane....Nonsense
Kwa iyo kwa akili yako unadhani tume ya mipango inasubirigi ilani ya Chama na ndo inapanga mipango???Tume ya mipango haikai tu na kuota kuwa tupange nini .hAWAINUI TU VICHWA HEWANI na kuja na mawazo toka angani kuwa tupange hivi!!
Yote huanzia kwenye chama kupitia ilani ambayo Raisi hukabidhiwa na chama kama mwenyekiti wa CCM taifa.Akishakabidhiwa yeye hukabidhi kwa wataalamu wake wachote humo waende nayo kutengeneza mipango ya taifa ndipo utaanza kuona mpango wa taifa unaibuka na lazima uwe na allignment na ilani ya chama tawala na sera zake ila kwa wewe karani ofisi ya mipangi huwezi jua origin yake sababu wewe ni mtu wa chini sana kwenye utendaji wewe unatupiwa tu kuwa brain storm from here!!
Akafungue nyingine aone kama sisi wananchi tutakuja.Kwanza tutakuja kufanya nini saa za kazi.Ni kweli huu ni ukatili na uonevu mbaya.Taratibu za kumsimamisha kazi mtumishi wa umma Tanzania jamani ziko wapi? Sasa hivi ni kufukuzana kazi tu bila kujali utu wa mtumishi wa Umma.This is the
This is the highest degree of stupidity na ni uonevu wa watumishi wa kiwango cha juu kabisa kuwai kutokea.
Bado natafakari kama nilichokiona hapa ni kweli kimetokea nchi ya Tanzania. Nchi inayojisifu kuwa nchi ambayo haina ubaguzi wa rangi, vyama na makabila. Nchi ambayo kiongozi wake muda wote akienda kanisani anashikaga mike na kusema kuwa nchi ya Tanzania tumtangulize Mungu.
Nasema tena huu ni uonevu wa kiwango cha juu kabisa niliowai kuushuhudia hapa Tanzania.
siku ukiwa vyeo vikubwa utaelewa mipango huanzia wapi kwa sasa endelea na u karani tume ya mipangoKwa iyo kwa akili yako unadhani tume ya mipango inasubirigi ilani ya Chama na ndo inapanga mipango???
Siendi tena kusoma kwakweliAnyway huyo manager hajui maana ya team work ilibidi awasiliane na viongozi wenzie kuhusu ujio wa waziri na kuwaalika rasmi kwenye uzinduzi na kuomba magari ya matangazo yazunguke mjini kutangaza uzinduzi nk
Vyeo vyote vya uteuzi ni vya kisiasa sababu raisi mfano huzunguka nchi nzima jua lake mvua yake mbu wake,VUMBI LAKE ,TOPE LAKE kutafuta kura kwa wananchi wakati hao watendaji huwa wako majumbani mwao wanakula viyoyozi kwenye ofisi na magari yenye VIYOYOZI
Raisi ambaye ni mwanasiasa akishaumia kwa yote hayo anasema ninakuteua ushike nafasi fulani halafu unaanza kujitia ohh mimi sio mwanasiasa sisikilizi wanasiasa huyo aliyekuteua ni nani? Akakufanya unakaa jumba kubwa yenye viyoyozi na gari yenye kiyoyozi .Bila huyo mwanasiasa ungekuwa hapo ulipo? TARURA yenyewe ilianzishwa na wanasiasa kwa sheria ya bunge iliyopitishwa na wanasiasa.Bila wanasiasa mtu angekuwa meneja wa TARURA?
Wanasiasa waweza hata kesho wakaamua kuifuta TARURA yeye atakuwa meneja wa wapi? Wanasiasa ndio wanawaweka mjini hao wanaojiita wataalamu watendaji.Wanatakiwa kuwa na adabu ya hali ya juu kwa wanasiasa
Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo amemuondoa kwenye nafasi yake Meneja wa TARURA Jijini Arusha, Podia Mwankenja kwa kushindwa kukusanya Wananchi kushuhudia barabara zilizokamilika alizokuwa akizitembelea.
Waziri Jafo amesema, “Mnataka Serikali ionekane haijafanya kitu wakati Wananchi ndio barabara yao? Kama ni barabara ya Wananchi mbona Wananchi hawapo hapa? Au unataka Serikali ionekane haijafanya kitu katika maeneo yao?”
Waziri Jafo amemuhoji Meneja huyo ambaye pia ndio Mratibu wa barabara za Jijini humo “Kwanini hii tunazindua barabara hii Wananchi hawapo? Unataka Rais aonekane hajafanya kitu? Rais ameweka fedha hapa. Mmeficha halafu kesho na kesho kutwa mseme Rais hajafanya kitu?”
Aidha, Meneja huyo alipoanza kujitetea na kusema kuwa alidhani Mtendaji (Mkurugenzi) amefanyia kazi suala hilo, Waziri Jafo alimwambia “Wewe si barabara zako? Unafanya sabotage ili Rais aonekane hajafanya kitu halafu kesho Wananchi waseme hakuna lolote Rais amefanya?”
Waziri Jafo amemalizia “Ninyi ndio wataalamu mnaofanga Serikali ionekane haijafanya jambo wakati sisi hapa Arusha tumewekeza fedha nyingi. Mji wa Arusha tumetandaza Barabara ila wewe unaficha hata Wananchi hapa jirani wasijue tumeweka barabara”
Huyo jamaa anajiaibisha muache mkuuKwa iyo kwa akili yako unadhani tume ya mipango inasubirigi ilani ya Chama na ndo inapanga mipango???
Usiku mwema mzee.
Yaani jafo huwa anaonekana ni mtu smart kumbe nae hamna kitu.Kwani hao wananchi hawaoni jamani hizo barabara? Sasa barabara utaifichaje? Halafu meneja kazi yake ni kuhakikisha kazi imefanyika kwa kiwango. Siyo kukusanya wananchi. Hii serikali ya sifa, hii...! Ngoja nikazane na biashara zangu tu.
Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo amemuondoa kwenye nafasi yake Meneja wa TARURA Jijini Arusha, Podia Mwankenja kwa kushindwa kukusanya Wananchi kushuhudia barabara zilizokamilika alizokuwa akizitembelea.
Waziri Jafo amesema, “Mnataka Serikali ionekane haijafanya kitu wakati Wananchi ndio barabara yao? Kama ni barabara ya Wananchi mbona Wananchi hawapo hapa? Au unataka Serikali ionekane haijafanya kitu katika maeneo yao?”
Waziri Jafo amemuhoji Meneja huyo ambaye pia ndio Mratibu wa barabara za Jijini humo “Kwanini hii tunazindua barabara hii Wananchi hawapo? Unataka Rais aonekane hajafanya kitu? Rais ameweka fedha hapa. Mmeficha halafu kesho na kesho kutwa mseme Rais hajafanya kitu?”
Aidha, Meneja huyo alipoanza kujitetea na kusema kuwa alidhani Mtendaji (Mkurugenzi) amefanyia kazi suala hilo, Waziri Jafo alimwambia “Wewe si barabara zako? Unafanya sabotage ili Rais aonekane hajafanya kitu halafu kesho Wananchi waseme hakuna lolote Rais amefanya?”
Waziri Jafo amemalizia “Ninyi ndio wataalamu mnaofanga Serikali ionekane haijafanya jambo wakati sisi hapa Arusha tumewekeza fedha nyingi. Mji wa Arusha tumetandaza Barabara ila wewe unaficha hata Wananchi hapa jirani wasijue tumeweka barabara”
Anasikitisha na kutia hasira kwa kweli. Sijui CCM iliingiliwa na nini kuwa na mijitu Kama yeye??Huyo jamaa anajiaibisha muache mkuu
Karibu Ruvuma tufanye kilimo ingawa sera za Chama chako kimenifanya nikose hela kwa kuzuia mahindi kuuzwa nje.siku ukiwa vyeo vikubwa utaelewa mipango huanzia wapi kwa sasa endelea na u karani tume ya mipango