Waziri Jafo amuondoa kwenye nafasi yake Meneja wa TARURA jijini Arusha kwa kushindwa kuita Wananchi kushuhudia ufunguzi wa barabara

Sikujua huyu mzaramo anakick za kipuuzi kiasi hicho
 
Hahahahahahahahah just hahahahahahaha kesho utasikia "sisi tunapendwa na wananchi, sijui wananchi wanampenda nani sijui"... Aibu gani hii kumbe huwa mnawasomba kwa maroli eeeeh!!?...


Sasa jafo, jiwe, na wengine wajue kwamba wananchi tumewachoka wasitulazimishe kufurahi bila sababu za msingi......

Unaweza kumlazimisha punda kwenda mtoni ila kamwe huwezi kumlazimisha kunywa maji
 
Hilo kosa ni la kumuondoa mtu kweli?Kwa taarifa yake watu kama yeye Jaffo ndio wanaosasabisha hii serikali ichukiwe kwa maamuzi kama haya
Halijui kama linawajaza watu hasira yaani mamtu ya Ccm sijui yanakula bangi ya wapi
 
Hii habari imeniuma sana....yaan mpaka sa iv kuna kitu kimenikaa hapa rohoni........alaf mzee anajaribu kujitetea anamkatisha makusud........nchi yangu unaelekea wapiiii????
 
Hii ndio sababu ya kumtoa mtu kazini.......this is Insane....Nonsense
Najiuliza...hivi kazi ya manager wa Tarura ni kukusanya wananchi kwenye ziara za rais au ni kazi ya Pole pole
 
Huu ni undezi wa kiwango stahiki, sasa si asingezindua,halafu hiyo maeneo ni njiro, kila mtu yuko bize, mchana watu wameenda maofisini, isitoshe ndio maeneo ya nyumbani kwa mbunge ambaye ni Godbless. Mi nafikiri angempigia Lema amwambie amtafutie wananchi.
Otherwise nafikiri kuna something fishy, given the fact that uongozi wa mkoa umeondolewa recently, labda meneja nae ni muhanga wa maugomvi ya former RC, DED na DC
 
Huyu mzaramo angalau wandengereko Wana akili kiduchu
Nitajie hata mndengereko mmoja tu aliye hata na diploma tu unayemjua anayejulikana .HUWEZI LINGANISHA MZARAMO NA MNDENGEREKO
 
Vyama vya wafanyakazi vinatakiwa kumkemea huyu wazili
 
Inawezekana kabisa kufanikiwa bila ya kutelemsha wenzetu. Alichokifanya Jaffo hakikubaliki duniani na mbinguni.
Anyway muda unayoyoma aendelee kuzunguka huku na kule kumsifia mwanaume mwenzake ili jamaa akiamka siku hiyo hasije akalisahau jina lake.
 
Pathetic! Job specifications za meneja wa TARURA ni kukusanya wananchi? Hapa mh Jafo hajatumia busara! Huo ni ulevi wa madaraka.
 
Jafo kadhihirisha ile tabia na Usanii wa CCM kusomba watu kwenye Ma Fuso ili kupata Nyomi
 

Huko ni kumuonea tu huyo meneja.
Kwani hizo barabara si zinaonekana tu hata kama wasingefika hapo? Je alitaka huyo meneja akawakusanye watu na kuwaleta kwa malori na mabasi kama wanavyofanya kwenye kampeni ili ionekane kuwa kulikuwepo na watu wengi?

Sioni sababu ya kumlazimisha mtu awepo wakati wa uzinduzi kwani kama hizo barabara zipo zipo tu hata kama watu hawakukusanyika.

Anaposema huyo meneja anaficha hizo barabara, je aliziweka mfukoni au amezificha wapi?
 
Jafo ni miongoni mwa ministers ambao nilikuwa nawaheshimu na kuwaona 'smart' kiasi fulani katika utekelezaji wa majukumu yao ya kiserikali.

Lakini kwa tukio hili, comrade Jafo umeanza kuwa na maamuzi mabovu... pengine ni ulevi tu wa 'madaraka'!

Meneja katekeleza majukumu yake barabara imejengwa.

Ila Meneja kushindwa kualika wananchi kwenye uzinduzi ndiyo unaitafsiri as 'sabotage' kwa Rais?!!! Kweli?

Msilewe madaraka na kujisahau sana mkiwa kwenye hivyo vyeo vya muda mfupi.

Just by common sense, huyo Meneja umemuonea. Karma itakushtaki kwa mwajiri wako.

Aliyekupandisha ndiye atakayekushusha pia. Tuweni na kiasi katika maamuzi.

-Kaveli-
 
Kuna kujipendekeza kupitiliza kiasi cha hadi kulazimisha hata watumishi wa umma wajipendekeze kwa wanasiasa. Ndiyo, anayetaka kujipendekeza rukhsa, lakini asiyetaka asilazimishwe kujipendekeza hadi kutishiwa kufukuzwa/kuhamishwa kituo cha kazi. Haifai! Mhandisi anayesimamia mradi wa kujenga barabara atahusishwaje na masuala ya kuhamasisha wananchi kwenda kumlaki/kushuhudia wanasiasa wakikagua barabara? Kama miaka mitano ya mwanzo ndio hii, miaka mitano ya lala salama itakuwaje? Wataalam wengi si watahama nchi?
 
Jaffo aondolewe kwa kosa gani? kosa ni la huyo meneja kushindwa kualika watu, hata kwenye harusi watu wasipohudhuria makosa ni ya waandaaji, sio wenye harusi.

Watu waje kufanya nn?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…