Waziri Jafo asema atabandika majina hata ya wale waliojitoa na kura zitapigwa

Hata Seif Sharif kwenye Uchaguzi wa marudio alitangaza kujitoa lakin hakutolewa kwenye karatasi za kupigia kura


Uchaguzi ni kama ndoa ya kikristo, kuingia rahisi ila kutoka sasa ...

Uchaguzi wa Zanzibar ni wa mkoa, ni tofauti na huu wa nchi. Huu doa lake linakuwa wazi zaidi kuliko uchaguzi wa mkoa wa Zanzibar. Tunashukuru hii hali imejitokeza sasa, yale madai yetu ya mgombea binafsi yapate ushahidi baada ya kuhujimiwa na ccm.
 

Mimi sio mwanasiasa na siipendi siasa lakini kwa namna ambavyo serikali inaendesha mambo haya wanatengeneza bomu kubwa sana mioyoni mwa watu. Na jambo hili linahitaji hekima kubwa sana.

Kujiengua kwa vyama vya upinzani wasichukulie mzahamzaha mimi naona kuna tukio kubwa sana linapangwa na hawa viongoz wa vyama.

Lakini pia Rais anapaswa afute uchaguzi huu hii ndio hekima pekee na asikilize matakwa ya vyama vyote maana wote ni wachezaji.

Ila akikaidi akaona ni jambo rahisi tuendako meli itazama yeye akiwa nahodha
 
.
 
Haijatumika demokrasia kuwakataza watu wasigombee

Mbowe anetumia ubabe
 
Mbowe kuwakataza watu kugombea ni demokrasia???
 
Haijatumika demokrasia kuwakataza watu wasigombee

Mbowe anetumia ubabe
Ni sisi wanachama tumemtuma, Ni ubabe gani alioutumia?
Kwani alipokuwa akitangaza CHADEMA kujitoa, alikuwa akitangaza akiwa chumbani kwake na mkewe?
Hamisha akili zako kutoka kisiginoni na kuzirejesha mahali pake, vinginevyo utajikuta unarudi nyuma Kila siku, Hadi utakuwaπŸ™‰πŸ™Š nyani, wakati watu tulushatoka huko long time kitambo
 
nchi inaendeshwa kwa utashi wa wenye mamlaka, kauli zao ndio katiba na sheria.
wao wanaweza kusamehe au kufiringa na kusambaratisha.
 

Ile idadi ya kubumba ya wapiga kura ndio chanzo cha yote haya au kwa kifupi tuseme "Ngoma imenasia"
 
Huyu siyo binadamu ni bonobo.
 
Watu wanagombeaje wakati majina yao tayari yamesha katwa?
Atakachofanya ni kuwa wameshinda rufaa wakati hata fomu zao hazionekani! Pia sasa wamechomekea kuwa na wagombea wa CCM nao wamekata rufaa kuonesha hakukua na upendeleo, propaganda za ajabu za enzi za kikomunisti!
 
Mbowe kuwakataza watu kugombea ni demokrasia???
 
mfano. wana chadema wote hawaendi kupiga kura kwa kuwa uongozi umeamua chama hakitashiriki. sasa huyo mgombea atapigiwa kura na nani?
Watawapitishwa tu wachache watakaoona kwao wanafaa,hata kama hana hata kura moja kwenye sanduku,atapishwa tu ili kujaribu kudanganya umma kwamba wapo na waupinzani waliopita. Na tutegemee lidubwasha kama hilo kwenye uchaguzi wa ubunge na udiwani 2020
 
Naona Kuna mihemko hapa kwa jafo;

Chama ambacho watu wake wameshindwa kujaza fomu, mnawalazimisha kuwashirikisha ktk uchaguzi wenu! Je mnauhakika Sasa wataweza kuandika mapingamizi Kama kujaza fomu kuliwashinda?

Waliojitoa achana nao, CCM big up sana mmeshinda kwa asilimia 100%.

Lakini kumbuka haki huinua taifa, na Mungu hadhihakiwi Kama mnakwenda misikitini na makanisani, halafu mnafanya haya tunayoyaona ! basi ni vema mkabaki kuwa wapagani tu maana mfanyayo ni ya kipagani.
Hakuna hofu ya Mungu ndani yenu.
Hakuna Utu ndani yenu
Hakuna ubinadamu ndani yenu
Hamuamini ktk ushindani
Mmeangalia yasiyowaheshimisha
100% CCM ishinde.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…