Waziri January Makamba anamaanisha Magufuli alikuwa akiwakatia umeme watumiaji wakubwa na kuwatisha wakae kimya?

Waziri January Makamba anamaanisha Magufuli alikuwa akiwakatia umeme watumiaji wakubwa na kuwatisha wakae kimya?

January Makamba akijibu hoja za wabunge kuhusu kukatika kwa umeme, kwanza alimlaumu mbunge Musukuma kwa kumshambulia yeye binafsi na kueleza kazi ya ubunge sio kushambuliana na kama ana matatizo na yeye kuwa waziri au samia kuwa rais apeleke kwingine lakini sio kwenye masuala ya nchi.

Pamoja na maelezo mengine, Makamba alitoa takwimu za TRA zinazoonyesha kipindi cha urais wa Samia suluhu na yeye akiwa waziri, makusanyo yamepanda, na kueleza hii inatokana na kuwa wao hawawakatii wenye viwanda umeme na kuwaambia wanyamaze ndio maana uzalishaji umepanda.

Makamba aliongeza pia matatizo ya kukatika kwa umeme yametokana na legacy, ambapo kipindi kilichopita repair and maintainance ilikuwa haifanywi ipasavyo, na akamaliza kwa kusema kama waziri aliyepita alipewa miaka 4, basi na yeye apewe miaka 4 waone kama hali ya kukatika itakuwepo na kama Magufuli walimpa miaka 6 basi na Samia wampe miaka 6 waone kama haya matatizo yatakuwepo

unajua mtu anaweza kuropoka siri bila kujua!! tulimpa miaka sita then ..........??? tukamuondoa ???
 
Acheni kelele.. Hii wizara ina changamoto nyingi na hazijaanza leo wala jana.

Too early kumjudge vibaya Makamba aliyepewa wizara muda mfupi uliopita.

Nasisitiza ni mapema mno apewe muda zaidi..
Kama analijua hilo kwa nini yeye anatupia mzigo wa lawama awamu iliyopita na Waziri aliyemtangulia? Tulidhani yeye amespecialize kwenye Conflict Resolution angekuja na jawabu la uhakika la "tatizo sugu la umeme" na si kutupia mzigo wa lawama wasiokuwepo.Muda hatumpi,aonyeshe '"umahili wake uliotukuka" katika kutatua hili tatizo.Vinginevyo akubali kuwa yeye kwa ile Wizara ni maji marefu kwake,aachie wenye uwezo washike Wizara hiyo.
 
Waziri Makamba yuko sahihi 100%. Bahati mbaya hatokei kambi ileeee inayomong'onyoka kila uchwao. Ame tabulate figures, facts walizoficha kina Kalemane kwa style ile ya kuambiwa ni fedha za ndani kumbe ni mikopo tuuu! JNHP imechelewa kwa siku zaidi ya 470 lakini Kalemani alisema maji yangeanza kujazwa Nov 2021. Ukweli ndio dawa ya kupona. Asante MakambabJnr. Piga kazi.
kwa hiyo kutabulate figures ndiyo kutatua tatizo la umeme? Hatuhitaji mbwembwe za makaratasi tunahitaji umeme wa uhakika,Period.
 
Kama analijua hilo kwa nini yeye anatupia mzigo wa lawama awamu iliyopita na Waziri aliyemtangulia? Tulidhani yeye amespecialize kwenye Conflict Resolution angekuja na jawabu la uhakika la "tatizo sugu la umeme" na si kutupia mzigo wa lawama wasiokuwepo.Muda hatumpi,aonyeshe '"umahili wake uliotukuka" katika kutatua hili tatizo.Vinginevyo akubali kuwa yeye kwa ile Wizara ni maji marefu kwake,aachie wenye uwezo washike Wizara hiyo.

Bro,
Hoja yangu ni kuwa tuache muda umprove incompetent for that post, kwa maana kuwa suala la kukatika umeme sio tatizo la waziri bali ni Technical reasons ukiwemo na kuongeza installed capacity ya uzalishaji nchini.
Kama atashindwa kusolve hizo challenges hapo itabidi aondolewe mara moja, ila kwa sasa it's too early tumpe muda.
 
Back
Top Bottom