Waziri January Makamba hana msaada wowote kwenye Wizara ya Nishati. Tumechoka!

HAPA JANUARY HACHAFULIWI BALI WATU WANATOA NYONGO YAO KUTOKANA NA ADHA WANAYOPATA KWA UMEME KUKATIKAKATIKA NAHIVYO KUATHIRI MAISHA YAO!! SABABU ANAZOTOA JANUARY ZA UMEME KUWA KERO HAZIRIDHISHI!!!
Hilo si limetolewa maelezo kwamba mfumo haukufanyiwa maintenance kipindi Cha magu wakiogopa kutumbuliwa!!..kwamba Kuna ufundi unaendelea,ukikamilika umeme utakua stable
 
Ndugu hata kama binadamu wote ni sawa .

Lkn huwezi kuwa sawa na life style ya waziri hata siku moja.
Ni kweli Binadamu hawapo sawa lakini mkishakuwa kwenye chumba kimoja matendo ya binadamu kiongozi mmoja yanakuhusu moja kwa moja wewe anayekuongoza.
 
Kalemani huwezi kumlinganisha na huyo February.

Kalemani ni mtu ya kazi sana naona mama walimdanganya sana
 
Labda kwenu, huku kwetu bushirombo hatuna shida ya umeme
 
Kukatika umeme kwa rate hiyo ni aibu kwa muda wa dunia ya sasa. Jana Posta nzima imeshinda haina umeme toka saa 3 MPAKA kumi watu wanaambaa hakuna stima kuanzia kisutu magistrates court, tanganyika library nk.

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Hiyo ndiyo ccm. Ni wajuzi wa kutengeneza tatizo bila kujali athari yake kwa wananchi, mkishaumia sanaaa, wanaleta mtu wa kulitatua , watanzania tulivyo na uwezo mdogo tunashamgilia huku tukipongeza na tukishukuru. Hapo wanakuwa wamewin. Kwa hili wala hutamsiki yule sijui shaka kama alivyohoji kwenye swala la machinga. Yupo kimyaaa! Watanzania tuamke tuache uvivu, tukatae huu ujinga. Inawezakanaje umeme toka asubuhi hadi usiku hakuna. Alafu si wizara, TANESCO ,wala mamlaka za nchi imejitokeza kuwambia watanzania tatizo. Bado tunaona ni kawaida.
Juzi mtendaji mmoja katika taarifa ya uwezekano wa kuishiwa mafuta , ajabu ni kwamba waziri kamtishia atoe maelezo! Only Tanzania.
 
Watu mmelipwa kiasi gani kumchafua?

Sio kwamba anachafuliwa, ila watu wanashangazwa na namna mambo yanavyoenda na sababu zinazotolewa kuhusu ukatikaji umeme

Alipokuwa Kalemani umeme ulikuwa hausumbui kwa kiwango hiki, lakini pía Kalemani kiukweli alikuwa mtu wa kujituma sana bidii yake ya kusambaza umeme kila pembe ya nchi tumeiona lakn pía Gharama za umeme kufunga umeme nazo zimeshuka

Ila alipoingia January ukatikaji wa umeme umekuwa wa kiwango kikubwa na pía sababu anazotoa eti mifumo ya Tanesco imechoka na ilishachoka toka enzi za Magufuli ila viongozi wake walikuwa waoga kutumbuliwa ndio maana haikufanyiwa ukarabati

Sasa watu wanajiuliza inamaana hadi mifumo ilikuwa inamuogopa Magufuli ndio maana haikuwa ikiharibika..!?????
 
HAPA JANUARY HACHAFULIWI BALI WATU WANATOA NYONGO YAO KUTOKANA NA ADHA WANAYOPATA KWA UMEME KUKATIKAKATIKA NAHIVYO KUATHIRI MAISHA YAO!! SABABU ANAZOTOA JANUARY ZA UMEME KUWA KERO HAZIRIDHISHI!!!
Mbolea elfub95 hatuwasikii wakilaumu ila January ukilala ukiamka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…