BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Waziri mpya wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Ukonga Dar es salaam @JerrySilaa ametangaza kusimamisha ujenzi holela wa Vituo vya mafuta Nchini Tanzania na kutaka ujenzi wowote unaofanywa kuanzia sasa kuzingatia sheria ya kutovisonganisha vituo.
Waziri Silaa ameyasema haya katika mkutano wake na Watendaji wa Wizara hiyo ikiwa ni siku yake ya kwanza Ofisini toka aapishwe kuwa Waziri ambapo amesisitiza kuwa Vituo vya ndani ya Mji kuwe na umbali wa mita mia mbili kati ya kituo kimoja hadi kingine.