Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Katika muendelezo wa kile waziri wa ardhi Jerry Silaa anachokiita kliniki ya ardhi na kutatatua changamoto za ardhi ameendelea kupuuza kabisa documents/nyaraka halali za serikali na mahakama za wale wanaodaiwa kuwa ni wavamazi au wanunuzi matapeli waliojimilikisha ardhi za watu wengine. Yani mtu ana hati yake halali ya umiliki kutoka serikalini anakuaje mvamvizi au tapeli wa kiwanja?!
Kwanza, swali la kwanza ni kwa vipi serikali inaweza kutoa hati zaidi ya moja kwa watu tofauti kwa eneo lile lile?
Pili, ni kwa nini hatuoni ukiwawajibisha maafisa ardhi na kamishna wa ardhi kwa namna yeyote ile tangu umeanza harakati zako?
Tatu, kuna maana gani sasa ya kwenda mahakamani kama waziri ndiye amegeuka kuwa mgawa haki?
Waziri Silaa anapaswa kujifunza kidogo katika iliyokuwa Libya ya Gaddafi, wakati Gaddafi akitawala Libya alianzisha sera ya kwamba umiliki haki na makazi ni mojawapo ya haki za msingi za kibinadamu za raia wote wa Libya. Sera aliipeleka vibaya sana kwa misingi ya kuwapa wanyonge makazi. Aliitaabishia, kuikatisha tamaa na kuifanyia vurugu makusudi biashara ya ardhi na makazi libya mpaka biashara ya real estate ikawa kama haipo kabisa.
Kwa sababu ya serikali kutoheshimu na kutotilia maanani nyaraka Ilikuwa ni kawaida wamiliki wa nyumba kuuza au kukodisha nyumba zao halafu baadaye wanageuka wanasema wamedhulimiwa. Waliokuwa wanyonge walikuwa wanavizia watu wenye nyumba zao wanaposafiri wote wanavamia nyumba wanavunja wanaigeuza ya kwao, mkirudi mnakuta nyumba ina watu wengine na haijalishi kama mna documents za kuthibitisha umiliki wenu nyumba au kiwanja mnaweza msipate tena, wao utetezi wao ni huo wa unyonge na haki ya kuwa na makazi, zaidi sana ukiwa tajiri mwenye nyumba nyingi ndio hakuna utakachoambulia kabisa wanyonge watakapodai baadhi ya nyumba yako.
Pamoja na matatizo makubwa yaliyopo katika sekta ya ardhi na makazi nchini, Jerry Silaa anapaswa kwanza kushughulika na mambo ya msingi ambao ni mfumo wa ardhi kuruhusu document za serikali zaidi ya moja kwa watu tofauti, maafisa ardhi na wengine wa serikali wanaotoa hizo nyaraka na pia aheshimu mahakama kama mtoaji haki wa mwisho, anachoweza kufanya yeye au serikali kusaidia ni kuzifanya mahakama zitoe maamuzi kwa haraka na kuwasaidia wanasheria wananchi wanaodai kudhulimiwa.