Anchoongea Waziri Katambi kwa maandishi
Kuna ambo wana kauli za ajabu kwenye vyombo vya habari. Tutachukua hatua pale mtaakapovunja sheria.
Lekini hatutaishia hapo tu. Na hii haivunji na haihusianii na kuvunja haki za binadamu na utawala bora, haihusiani na kuvunja misingi ya haki za binadamu kwa maana ya uhuru wa kujieleza. Lekini tusiutumie uhuru wetu wa kujieleza kuvunja sheria, kupotosha na kesema uongo.
Wapo watu ambao leo — sitawataja hadharani hapa kwa sababu lazima tutachukua hatua — wapo watu ambao wametoa takwimu za serikali za uongo. Na tunayo sheria ya takwimu.
Tuna watu ambao wametoa maelezo juu ya mambo na mipango na utekelezaji wa majukumu ya serikali kwa uongo, isivyo uhalisia.
Lekini matokeo yake yanaleta taharuki kwa wananchi, matokeo yake maneno yake yanaleta ubaguzi kwa wananchi, na hata pale viongozi wa serikali walivyokwenda kumwonyesha takwimu halali, akasema anaomba radhi; hakurudi kwenye vyombo vya habari kwenda kukanusha.
Sasa ukifanya mizaha mizaha hii, tunaenda kuangamiza taifa letu, tunapoteza amani. Ni kwa sababu siku hizi tunaona aibu kusimamia sheria. Kwa sababu siku hizi tunaona aibu mtu anayesema jambo la haki na kweli, tunaona kama anakosea.
Lazima turudi katika misingi ya haki, sheria, taratibu na kanuni. Na sisi hatutasita kuchukua hatua.
Kwa hiyo niombe sana, mizaha mizaha — tuzungumze jambo kwa kweli na kwa haki na kwa utaratibu ambao umewekwa kisheria. Uhuru wa maoni, uhuru wa kujieleza, uhuru wa kutoa habari na kuwashana habari upo kwa mujibu wa ibara ya 18. Tutaisimamia kwa wivu mkubwa ili haki hiyo iendelee kuwepo. Lekini tusiutumie uhuru tulionao kwenda kuliangamiza taifa letu.
Kwa hiyo leo ikiwa ni siku maalum ambayo tunaitumia kuhakikisha kwamba tunatoa amnesty au msamaha, uhuru wa watu ambao wanamiliki silaha isivyo halali kuziwasilisha kwa usalama, lakini pia inatupa fursa ya sisi kujikagua kwenye maeneo mengine ya kiusalama ili jambo lisiwe moja kwa ajili ya kuhakikisha kwa ujumla nchi yetu inakuwa salama.
Hivyo pia hata vyombo vya habari ninavyiomba: tusirushe maudhui ambayo tunaona haya yanalibagua taifa, yanalipasua, yanaleta nyufa. Tunayo sheria ya Media Content Regulation..."