Waziri Kigwangala ikuingie kichwani kwako, Wanyama, Mbuga hazileti Watalii!

Nani alikudanganya Misri hawana beaches?

dodge
 
nadhani serikali inewahasisha wawekezaji kuwekeza kwenye sekta ya kula bata kwa kuwapa feva km vile msamaha wa kodi nk.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu usichanganye chuki yako kwa Zito na uzi huu, jadili hoja.
 
Unakaa siku ngapi kwa hiyo hela? Mwaka?
Hapana hicho ni kiasi unachoweka reserve ukibook ticket, bei ni milioni 57 kwa siku minimum siku 5 hivyo uandae zaidi ya milioni 250 kwa siku utakazokaa. Baadhi ya vitu unavyopata ni kama
-usafiri wa hellcopter bure toka dar ama mafia
-kuogelea na papa
-uvuvi wa chini ya bahari samaki wasiopatikana rahisi juu
-facilities kama gym, Tennis, beach volleyball etc
-spa
 
Hii dunia kweli inaliwa na wenye pesa, just 5 days unatumia mil 250 ? Kweli Mimi ni masikini!
 
Znz kuna vitu unique vinavyopatikana kwao tu.
-vyakula mbalimbali kama muhogo wa Nazi, ndizi za bokoboko, supu ya pweza, mashelisheli etc
-kobe wakubwa sana
-biashara ya watumwa
-utamaduni
-vipepeo etc

Unawakuta wazungu beach, wengine sauti za busara kama unavyosema ila primary aim ya kuja pale sio hio, kwao hio ni bonus tu.

Ni kama wewe uende mwanza kikazi then kuwe na Tamasha la Diamond uende then lile tamasha watu wajae kupita maelezo haitamaanisha ulienda mwanza kuangalia Diamond.
 
Hii dunia kweli inaliwa na wenye pesa, just 5 days unatumia mil 250 ? Kweli Mimi ni masikini!
Ukiangalia minada ya wachina ya Jade ama wazungu/waarabu kwenye picha ndio akili itafunguka zaidi, watu wananunua vitu vya ajabu kwa mabilioni/matrilioni ya hela. Juzi hapa picha ya bikra maria imeuzwa trilioni 1, hivyo huyo mtu ukimwambia milioni 250 hata hajali.
 
Trillion Picha? You must be lying!
 
Mbona hapo mnazungumzia Mzungu mzungu... Hamumgusii kabisa mbongo. .. Kwamba sisi ndio hatutaki kutalii.. .

Mkuu wabongo hatuna uwezo wa kutalii, sisi bado tuko kwenye hatua za matumizi ya choo na kunawa mikono baada ya kutoka chooni.
 


Hapo unachanganya mambo, Tanzania ni third World Country, Watalii wanaokwenda Paris au Gran Canyon huwezi kuwaleta TZ hakuna hiyo Miundombinu, hao ni Muzungu au Wajapani Upper middle class na upper class huko wana standard zao ambazo sisi hatuwezi kuzitimiza hapa Bongo hata Hospitali tu ya maana akipata seizure hakuna, ndo maana nchi masikini kama zetu ni lazima tutageti wale middle class na hata lower middle class kwani huku kwetu bado ni matajiri, ukiwajaza hata wanafunzi tu wa first world country kwenye bonge la festival moja Bagamoyo wataacha hela ndefu sana, na hao hawataki mengi kuwe na mpangilio mzuri, usalama kusiwe na vibaka beach basi.
 
Kwa nini unawaza kufeli tu?

Ndio maana nimesema tuimarishe miundo mbinu nikimaanisha Barabara, viwanja vya Ndege, Hospitali, Hoteli za nyota 5 n.k...hakuna kinachoshindikana.

Ni kujipanga tu, hata hao Matajiri wanataka kuona Simba na Twiga...ni kuwahakikishia tu thamani ya kuja kwao.
 


Kuimarisha Miundombinu kufikia ya Paris haiwezekani kwa Tanzania ya sasa hata kama tukifanya kila kitu sawa kwa miaka 10 mfululizo kuanzia sasa, hao AK tu wametuzidi sana tu lkn bado hawafikii hata robo ya Watalii wanaofika Paris.

Shida kubwa ya Utalii wa Tanzania kwa maoni yangu uko aghali sana lkn hakuna Miundo mbinu ya kuhalalisha hizo gharama, mfano mdogo tu Mlima Kili hakuna hata helicopta ya uokoaji iwapo mpandaji akiugua ghafla juu anashushwa na machela, sasa watu upper class wanajali sana vitu kama hivyo, huwezi muweka kwenye machela Tahiti karne ya 21.

Hawa hawa Backpackers tungewatageti wangeacha hela nzuri tu, ...
 
Hii dunia hata kusema tunasindikiza haifai, Sababu ukisindikiza watu kama hawa angalau na wewe uambulie chochote, a price tag of USD 450M? And we breath the same air? This is more than unfair, hawa watu wana sh ngapi to spend all that money on the artifact? Bank amebakiza sh ngapi? God have mercy.
 
hao hata kwenye forbes wameondolewa, sababu utajiri wao haupimiki, for comparison kampuni yenye thamani kubwa duniani ambayo hisa zake zinauzwa ni Apple, ina thamani ya dola trilioni 1 , ila Saudi Aramco ina thamani ya dola trilioni 2.

watu kama hawa ndio unawatega na vitu unique zaidi, kutoa budget ya wizara ni kawaida kwao
 
Wanatakatisha pesa hao mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu usichanganye chuki yako kwa Zito na uzi huu, jadili hoja.
Tatizo watu huwezi kujua maudhui ninayoongelea ,baada ya kuona jina la Zitto umeanza kuleta siasa,unapoongelea kitu ili kilete maana zaidi unaleta na milinganisho ya mada na madhara yake,ndio maana hatawanasheria hutoa mifano ya vifungu ambavyo hata si kama vya kesi inayohusika hutumia kuelezea madhara ya nadharia ili kuelezea maana husika,Elimika si ukariri tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…