Suala la Utalii ni suala zaidi la nyie Wahusika kujipanga, bila kujali ni kivutio gani kipo nchini kwako.
Mamilioni ya Watu wanatembelea Eiffel Tower (mnara wa Paris) kuliko hata fukwe nyingi maarufu au matamasha maarufu yaliyopo duniani...ni wewe ndio ujiulize kuna nini maalum kwenda kuona Eiffel Tower na si Ngorongoro au Serengeti?
Moja ya mambo wanayozingatia Watalii ni usalama na miundo mbinu, kuanzia usalama wa Mtu kama Mtu na usalama wa eneo husika.
Kwa mfano wakati ule Michael Jackson alikataa kwenda kati ya Ngorongoro au Serengeti sikumbuki vizuri, aliahirisha baada tu ya kuona miundo mbinu sio rafiki na rahisi kwa yeye kufika kule.
Sio vibaya tukawekeza kwenye huo Utalii wa fukwe, matamasha n.k, lakini tusije tukapotezea vile vitu adimu tulivyonavyo...wanasema 'stand out of the crowd' hizo fukwe na matamasha yapo sehemu nyingi, lakini Serengeti, Kilimanjaro, Ngorongoro zipo Tanzania pekee.
Tuwekeze kwenye kusambaza taarifa na kuboresha miundo mbinu, Mtu apate taarifa sahihi na uhakika kwamba akija anapata alichotarajia walau kwa asilimia 80.