Waziri Kigwangalla aagiza kampuni ya Uwindaji ya OBC ya Loliondo kurudi walikotokea kabla ya Januari 2018

Nchi huru, wanyama wanatoroshwa mchana kweupe, basi huo uhuru wanafaidi viongozi tu. Namshukuru kigwa kuigusa ortelo
 
Hata makinikia mlisema hivyo mwisho wameanza kulipa baada ya kubanwa
 
Mwarabu hapo anakaa kiholela au ana mkataba?
Tusubiri utekelezaji!
 
Kigwangwalah anawatisha tu anakata apewe mlungula na waarabu hana lolote.
 
Reactions: SDG
Hapo sasa ndo tulipoona udhaifu wa Mwinyi. Ni kama waarabu walirudi kuja kumega nchi wanavyotaka. Ungeweza kuona udhaifu wa akili ya mwafrika kuamini kwamba mwaarabu au mzungu akiwa hapa ni sifa fulani, vile!
 
Reactions: SDG
Huyo mwarabu ni mshenzi sana amewafanya vibaya sana vijana anaowakuta kwenye eneo lake. Hii ishu ilimuondoaga Mrema kwenye uwaziri ilipaswa kuanza NA mzee Mwinyi ndiye alimpa kibali cha kuwinda
 
Reactions: SDG
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla amesema siku za kampuni ya Ortello Business Cooperation (OBC) inayomilikiwa na Falme za Kiarabu kuendelea kuwapo katika Pori Tengefu la Loliondo wilayani Ngorongoro zinahesabika.


Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ololosokwani, Dk Kigwangalla alisema mgogoro wa Loliondo uliodumu kwa zaidi ya miaka 26 sasa utapatiwa suluhu na Serikali.

“Naomba wananchi muwe watulivu Serikali yenu inafanyia kazi matatizo ya Loliondo na kuhusu kampuni ya OBC kama ambavyo nilitaka leseni ya umiliki wa kitalu hiki ikimalizika mwezi Januari hatutawapa nyingine,” alisema.


Alisema kuna sababu nyingi za kutotoa leseni kwa kampuni hiyo ikiwamo kukiukwa kwa sheria ya vitalu ambayo hairuhusu kutolewa leseni katika eneo lenye mgogoro na pia ina eneo kubwa la kilomita za mraba 4,500 ambalo hawalitumii lote kutokana na kuwapo kwa makazi ya watu.


Akizungumza katika kikao hicho, mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Ololosokwani ambacho kinapakana na kitalu cha OBC, Koya Timan alisema kampuni hiyo ambayo inapakana na Hifadhi ya Serengeti imekuwa ikiwazuia wafugaji kupata malisho na maji.
 
Ivi watz wote tukiziunga mkono jitihada za serkal, tutafanikiwa fasta, bt serkal inatupigania while kunawatu wengine kazi yao ni kupinga na kuupotosha ukweli.
Ni kwa sababu unatofautiana nao katika uelewa na upataji taarifa!
 
Na wananchi waliouwawa na kuchomewa nyumba zao atawashurutisha wawalipe fidia?

Hebu tusubiri wangapi wataitwa kwenye hili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…