Waziri Kigwangalla aagiza kampuni ya Uwindaji ya OBC ya Loliondo kurudi walikotokea kabla ya Januari 2018

Waziri Kigwangalla aagiza kampuni ya Uwindaji ya OBC ya Loliondo kurudi walikotokea kabla ya Januari 2018

Mkuu hii ni nchi huru na mamlaka kamili. Hicho unachosema sio sahihi. Huwezi ukaruka na ndege bila ukaguzi kwenda nje ya nchi. Lazima upitie katika viwanja vya kimataifa km kia. Kwasababu ndege huwa lazima zipate clearance hata ya kupita tu katika anga ya nchi husika sembuse kutua na kuruka.
Nchi huru, wanyama wanatoroshwa mchana kweupe, basi huo uhuru wanafaidi viongozi tu. Namshukuru kigwa kuigusa ortelo
 
haya mambo yashatokea zaamani miaka ya 70 azimio la Arusha , tukapigwa vita tukawa hatuna hata sabuni , tunarudi tena kwenye mambo hayo uwezi kuyanganya vitu vya watu wakati walipewa na serikali ya ccm ?. mwishowe tutakwenda mahakamani kulipa fidia kesho wanaweza kuchukua mali za wafanya biashara za wazalendo
Hata makinikia mlisema hivyo mwisho wameanza kulipa baada ya kubanwa
 
Mwarabu hapo anakaa kiholela au ana mkataba?
Tusubiri utekelezaji!
 
Kigwangwalah anawatisha tu anakata apewe mlungula na waarabu hana lolote.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Waziri wa Maliasili asili na utalii Mh. Kigwangala akiwa katika ziara yake wilayani Ngorongoro pamoja na kuagiza kuvifuta vibali vyote vya uwindaji nchi nzima ikiwamo vya kampuni ya ORTELLO BUSINESS CORPORATION (OBC) ya Loliondo, ameagiza kampuni hiyo ya MWARABU kujiandaa kurudi walikotokea, kwasababu hata kama wakibaki mchakato mpya wa ugawaji vitalu vya uwindaji utakapoanza hautawahusu.

Ikumbukwe kampuni ilipewa eneo hilo miaka ya 1990 kwa mkataba wa miaka 99.
Hapo sasa ndo tulipoona udhaifu wa Mwinyi. Ni kama waarabu walirudi kuja kumega nchi wanavyotaka. Ungeweza kuona udhaifu wa akili ya mwafrika kuamini kwamba mwaarabu au mzungu akiwa hapa ni sifa fulani, vile!
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Huyo mwarabu ni mshenzi sana amewafanya vibaya sana vijana anaowakuta kwenye eneo lake. Hii ishu ilimuondoaga Mrema kwenye uwaziri ilipaswa kuanza NA mzee Mwinyi ndiye alimpa kibali cha kuwinda
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla amesema siku za kampuni ya Ortello Business Cooperation (OBC) inayomilikiwa na Falme za Kiarabu kuendelea kuwapo katika Pori Tengefu la Loliondo wilayani Ngorongoro zinahesabika.


Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ololosokwani, Dk Kigwangalla alisema mgogoro wa Loliondo uliodumu kwa zaidi ya miaka 26 sasa utapatiwa suluhu na Serikali.

“Naomba wananchi muwe watulivu Serikali yenu inafanyia kazi matatizo ya Loliondo na kuhusu kampuni ya OBC kama ambavyo nilitaka leseni ya umiliki wa kitalu hiki ikimalizika mwezi Januari hatutawapa nyingine,” alisema.


Alisema kuna sababu nyingi za kutotoa leseni kwa kampuni hiyo ikiwamo kukiukwa kwa sheria ya vitalu ambayo hairuhusu kutolewa leseni katika eneo lenye mgogoro na pia ina eneo kubwa la kilomita za mraba 4,500 ambalo hawalitumii lote kutokana na kuwapo kwa makazi ya watu.

pic%2Bkigwangala.jpg

Akizungumza katika kikao hicho, mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Ololosokwani ambacho kinapakana na kitalu cha OBC, Koya Timan alisema kampuni hiyo ambayo inapakana na Hifadhi ya Serengeti imekuwa ikiwazuia wafugaji kupata malisho na maji.
 
Ivi watz wote tukiziunga mkono jitihada za serkal, tutafanikiwa fasta, bt serkal inatupigania while kunawatu wengine kazi yao ni kupinga na kuupotosha ukweli.
Ni kwa sababu unatofautiana nao katika uelewa na upataji taarifa!
 
Na wananchi waliouwawa na kuchomewa nyumba zao atawashurutisha wawalipe fidia?

Hebu tusubiri wangapi wataitwa kwenye hili
 
Back
Top Bottom