Waziri Kigwangalla aagiza kampuni ya Uwindaji ya OBC ya Loliondo kurudi walikotokea kabla ya Januari 2018

Waziri Kigwangalla aagiza kampuni ya Uwindaji ya OBC ya Loliondo kurudi walikotokea kabla ya Januari 2018

Miaka ya '90 mwanzoni 'Loliondo gate' ilikuwa moto kweli. Ndolanga-kumtandika ngumi Qaresi(Mb). Enzi ya mzee ruksa
 
Yan katika wizara nilikuwa naomba kila siku muujiza wa namna hii utokee basi ni wizara hii ya maliasili na Utalii maana nafikiri hata wanyama wa maeneo ya loliondo watakuwa wamefanya sherehe baada ya kusikia hilo Bango la mmh.waziri kwa sababu ilikuwa imefikia hatua wanyama wanaopakana na hili Pori la Loliondo wamekuwa waoga sana waonapo magari ya Utalii na watalii wakiiinua camera kupiga picha wanyama walikuwa wakitimua Mbio kwa kudhani wanataka kupigwa risasi: kwa ufupi huu uwindaji umefanya wanyama kuishi kwa wasiwasi sana kutokana na kuuwawa hovyo na hawa waarabu. Hongera waziri ila ni matumaini yangu kuwa utafuta biashara ya uwindaji wanyama Pori kabisa ili tubaki na Utalii wa kutembelea na kuona wanyama na sio kuwauwa: we better shoot animals by camera not by gun..
Huyu hafanyi commercial hunting, huwa anakuja Mfalme wa Dubai kupumzika tu. Katika lile pori kengele za ngombe zinafukuza wanyama pori kuliko Milio wa risasi. Lakini as the saying if u want to kill a dog give it a bad name!
 
Tatizo letu watanzania huwa tukishakuwa excited hata kufikiri hatutaki. Nnavyoelewa hii issue siyo rahisi hivyo. Kwasababu hiyo kampuni haifanyi biashara. Ipo hapo kwa ajili ya kurahisisha safari za mapumziko ya ukoo wa kifalme wa Emirates. Na kama ni kweli muda wa kuwaondoa umefika approach ya waziri ni mbaya mno kwa mahusiano ya kidiplomasia. Kumbukeni Tanzania sio kisiwa. Kama tunategemea kuheshimiwa kwa viongozi wetu wa kitaifa basi tunapaswa na sisi tuwaheshimu viongozi wa mataifa mengine.
Heshima ya kuibiwa inakusaidia nn?? Bora udhalauliwe kwa msimamo wako, kuliko unakaa na jamaa ndani mwako anakugongea mkewo, anakula kila kitu chako na ww unaogopa kumfukuza kisa udumishe heshima na undugu.
 
Alimshughulikia tapeli Mwaka mpaka kahama nchi !
Hivi yuko wapi yule jamaa, alijitia jeuri naona kapotea mazima daaah haya maisha kweli noma, jamaa alikuwa anapiga hela chafu hadi basi!
 
Hivi yuko wapi yule jamaa, alijitia jeuri naona kapotea mazima daaah haya maisha kweli noma, jamaa alikuwa anapiga hela chafu hadi basi!
Nasikia yuko South Africa, kule nako wajinga wajinga wengi tu....!
 
Tatizo letu watanzania huwa tukishakuwa excited hata kufikiri hatutaki. Nnavyoelewa hii issue siyo rahisi hivyo. Kwasababu hiyo kampuni haifanyi biashara. Ipo hapo kwa ajili ya kurahisisha safari za mapumziko ya ukoo wa kifalme wa Emirates. Na kama ni kweli muda wa kuwaondoa umefika approach ya waziri ni mbaya mno kwa mahusiano ya kidiplomasia. Kumbukeni Tanzania sio kisiwa. Kama tunategemea kuheshimiwa kwa viongozi wetu wa kitaifa basi tunapaswa na sisi tuwaheshimu viongozi wa mataifa mengine.
Hujaelewa kidogo kwa sababu OBC unaisoma kwenye magazeti tu. Ni kwamba wanawinda mkuu......
 
Kama atafuata sheria zote za kuwaondoa,niko tayari kumuunga mkono.Lakini kama ndiyo yale magumashi ya kuja kutufanya tushitakiwe na kulipa fidia,bora aendelee na mengine tu.
 
Sitaki sikia hizi siasa uchwara. Toka kwa wanasiasa uchwara.

Swali la msingi huyu mtu anaepewa kauli kama hii je ni mvamizi wa ardhi yetu?

Na je sheria zetu hazikuhusika kwa kumpatia hiyo miaka 99?.

Tufuate utararibu wa kisheria tuache kutafuta popularity zinazowalaghai watantania.

Mlianza na ACACIA MINING COMPANY kuwaita wezi na kauli nyingi mbovu kana kwamba ni watu waliokuja na kukuta aridh haina mtu tokea kuumbwa. Mwishoni wezi hao hao mnakaa nao meza moja tena kwa miezi kadhaa mkiwaomba kuwafuta aibu ambayo kimsingi ninyi kama chama tawala ndio chanzo cha kuliingiza taifa katika migogoro ya biashara za kimataifa.

Rai yangu kwa viongozi wetu jitahidini kuwaheshimu wananchi.

Siasa zenu ziheshimu watu wote bila kujali utaifa na mkubali kuwa serikali ilikosea sana na tena kwa miaka mingi na leo jambo la msingi la kufanya ni kufuata maamuzi ya kisheria. Mmalize mambo yenu kwa approach ile ile kama mliyoitumia kuwakaribisha. Sio kutupigia kelele tuone kama una uchungu kumbe ukurupukaji tupu. Shame on you kigwangala.
 
Mimi binafisi sijawahi amini uwezo wa kigwangala toka akiwa afya. So tusubirie kusikia mengi ya hovyo.
 
Huyu hafanyi commercial hunting, huwa anakuja Mfalme wa Dubai kupumzika tu. Katika lile pori kengele za ngombe zinafukuza wanyama pori kuliko Milio wa risasi. Lakini as the saying if u want to kill a dog give it a bad name!

duh!
mkuu so zile video za wafalme wakiwwinda wanyama tena watoto na wenye mimba ni za kuedit au sio tz ?
 
kama wana ni ya dhati, wangeenza na walioingia mikataba, waliowapa vitalu, waliowamilikisha ardhi, waliopewa bahasha kwa namna yoyote ile!! halafu warudi kwa OBC wakimkuta pale loliondo bado yupo, wawaambie wananchi wachukue ardhi yao!!
 
Ivi watz wote tukiziunga mkono jitihada za serkal, tutafanikiwa fasta, bt serkal inatupigania while kunawatu wengine kazi yao ni kupinga na kuupotosha ukweli.
Serekali za ccm zina ujasiri wa kukosea katikati ya kelele, huo huo ujasiri utumike kufanya sup. zao.
 
duh!
mkuu so zile video za wafalme wakiwwinda wanyama tena watoto na wenye mimba ni za kuedit au sio tz ?
Hujanielewa. Anaewinda kwa biashara atahakikisha kuwa anafanya kila njia ili asipate hasara kwasababu ndo njia yake yakujipatia kipato. Huyo anaeitwa mwarabu ni mfalme wa Dubai. Kuja kwake huku kwetu sio kutafuta pesa bali anakuja kupumzika. Jaribu kufanya research juu yake. Huwa anaenda kufanya ziaraza utalii katika nchi nyingi sio Tanzania tu.
 
Kama kweli akitekeleza itakuwa ni faraja kwa wanaharakati wa mazingira, na wananchi wa maeneo hayo. Kimekuwa ni kilio cha miaka mingi.

Binafsi JPM akifanikiwa hili nitaamini kuwa hata kwenye makinikia alikuwa na nia njema, iwe amefanikiwa au hakufanikiwa.
Mimi pia mkuu!! Akifanikiwa kumwondoa huyu na wengine kadhaa wa aina hii basi kweli nitaamini kuwa sasa nchi inarudi kwa wenye nchi!
 
Tatizo letu watanzania huwa tukishakuwa excited hata kufikiri hatutaki. Nnavyoelewa hii issue siyo rahisi hivyo. Kwasababu hiyo kampuni haifanyi biashara. Ipo hapo kwa ajili ya kurahisisha safari za mapumziko ya ukoo wa kifalme wa Emirates. Na kama ni kweli muda wa kuwaondoa umefika approach ya waziri ni mbaya mno kwa mahusiano ya kidiplomasia. Kumbukeni Tanzania sio kisiwa. Kama tunategemea kuheshimiwa kwa viongozi wetu wa kitaifa basi tunapaswa na sisi tuwaheshimu viongozi wa mataifa mengine.
Kama wao hawatuheshimu hakuna haja ya kuwaheshimu!! Niambie mtanzania anayemiliki rasilimali huko arabuni kwa mkataba wa 99years! Siipendi ccm ila kwa hili nipo na yeyote mwenye kuonyesha nia ya kuwaondoa hawa ngedure nchini mwetu!
 
Hakika jamiiforums imenisaidia na inaendelea kunisaidia.

Inanijuza mambo mengi sana.
Yaani mtu anaingia mkataba wa miaka 99? Ama kweli hii nchi inaliwa na wengine kabisa
 
Back
Top Bottom