Waziri Kigwangalla aagiza kampuni ya Uwindaji ya OBC ya Loliondo kurudi walikotokea kabla ya Januari 2018

Waziri Kigwangalla aagiza kampuni ya Uwindaji ya OBC ya Loliondo kurudi walikotokea kabla ya Januari 2018

Huyo mwarabu ndo tunaambiwa huku JF kuwa hilo eneo lake ana mtandao binafsi wa simu?
Na hii ishu ndo iliondoa uhai wa Stan Katabaro?
pasco
Yaani hao mashaitwan walitutesa Sana afadhali sasa CCM wameanza kuvaa viatu vya CDM!
 
Sijapata kuona waziri jasiri kama huyu ktk wizara hii toka nimepata kujitambua. Big up @
KIGWANGALA.
 
Waziri wa Maliasili asili na utalii Mh. Kigwangala akiwa katika ziara yake wilayani Ngorongoro pamoja na kuagiza kuvifuta vibali vyote vya uwindaji nchi nzima ikiwamo vya kampuni ya ORTELLO BUSINESS CORPORATION (OBC) ya Loliondo, ameagiza kampuni hiyo ya MWARABU kujiandaa kurudi walikotokea, kwasababu hata kama wakibaki mchakato mpya wa ugawaji vitalu vya uwindaji utakapoanza hautawahusu.

Ikumbukwe kampuni ilipewa eneo hilo miaka ya 1990 kwa mkataba wa miaka 99.
Safi waziri kigwangalah kwa uthubutu huu, hakika tukiwa na mawaziri wa aina hii 10 basi nchi itafika mbali.

Sent from my SM-A520F using JamiiForums mobile app
 
Waziri wa Maliasili asili na utalii Mh. Kigwangala akiwa katika ziara yake wilayani Ngorongoro pamoja na kuagiza kuvifuta vibali vyote vya uwindaji nchi nzima ikiwamo vya kampuni ya ORTELLO BUSINESS CORPORATION (OBC) ya Loliondo, ameagiza kampuni hiyo ya MWARABU kujiandaa kurudi walikotokea, kwasababu hata kama wakibaki mchakato mpya wa ugawaji vitalu vya uwindaji utakapoanza hautawahusu.

Ikumbukwe kampuni ilipewa eneo hilo miaka ya 1990 kwa mkataba wa miaka 99.
Ni kweli kabisa tunahitaji mali zote za wananchi ziwe mikononi mwa wanaznchi wenyewe, na kama wapo waliokodishiwa kihalali kabisa wamefuata taratibu zote, ni vema sana tena itakuwa ni busara tukae nao tuongee nao pia tupate ushauri kwa wataalamu wa sheria akiwemo Jaji mkuu, waziri sheria na katiba na wangineo ili kuepuka kuja kulipa faini kubwa.
 
Hao waarabu wa Loliondo walimilikilishwa hilo eneo kisheria na serikali(Hata kama sote tunajua Rushwa ilitembea), tena umiliki wake ni wa miaka 99, Hivyo mkataba wao kisheria utaishia kwenye mwaka 2080 hivi.
Sasa kuwanyang'anya kienyeji enyeji haiwezekani, lazima iwe kisheria.

Kauli ya Kigwangwalla ni kauli ya kupuuzwa tu(japokuwa sote tunajua ni Magufuli mwenyewe huenda labda kamtuma kwenda kusema hayo ili kuleta choko choko).
Ngoja tusubiri, muda utatupa majibu.
 
Kwa maamuzi hayo hata mimi namuunga mkono ila ifanyike hivyo na isiwe maneno tu halafu baada ya miezi kadhaa tunaambiwa hiyo kampuni ya Mwarabu inaendelea tena kwa mkataba hulehule OBC )
 
Duuhh!! Hii imekaa viba mkataba wa miaka 99 inamaana hapo mkataba c unavunjwa vipi kuhusu fidia
 
Ivi watz wote tukiziunga mkono jitihada za serkal, tutafanikiwa fasta, bt serkal inatupigania while kunawatu wengine kazi yao ni kupinga na kuupotosha ukweli.

are you serious!?? kuunga mkono ndi nini na tunaungaje, tukiunga tunahusikaje?
 
Hapa tuwe wazalendo, tu fight for our natural wealth, sio kusema tuone kama wazir ataweza kuwafukuza, tumuunge mkono ndio tutapata mafanikio,
Je tumewapa masharti yetu wameshindwa kutimiza ?? Tukisha nyanganya !! What next ?? Je nini dhumuni la kunyanganya ?? Isijekuwa tunacheza mchezo wa Acacia na Barrick ili kutengeneza jina kisiasa kwa matamko ya kinafki. Time will tell.
 
Ivi watz wote tukiziunga mkono jitihada za serkal, tutafanikiwa fasta, bt serkal inatupigania while kunawatu wengine kazi yao ni kupinga na kuupotosha ukweli.
Tatizo kubwa kwa sisi waTz tulio wengi tunajua zaidi kukosoa ili mtu fulani aonekane kakosea, hajui, au ni mjinga. Ni watanzania wachache sana huenda kwenye media ili kutoa ushauri tena katika lugha nzuri na ya kizalendo ya kuonyesha kweli mtu anajali watanzania wengine na maendeleo ya nchi.

Wengi hutumia media mbalimbali katika kukosoa na sio kushauri, na ikumbukwe mtu anapokosea huenda hajui anahitaji kueleweshwa au amepitiwa hakuwa makini anahitaji kukumbushwa.
Sasa inapofika kipindi unamuattach nayeye anajibu na kufanya jambo kwa kushindana na wewe mkosoaji na sio kusikiliza ushauri wako.

Na tabia ya kushindana na mkosoaji sio tu kwa viongozi hata katika maisha yetu ya kila siku mtu akija akakukosoa kwa jazba na lugha ngumu ni jambo ambalo mara nyingi halivumiliki, wengi wetu tunakosa busara ya kutoa ushauri zaidi tunajua kuattach.
 
Hao waarabu wa Loliondo walimilikilishwa hilo eneo kisheria na serikali(Hata kama sote tunajua Rushwa ilitembea), tena umiliki wake ni wa miaka 99, Hivyo mkataba wao kisheria utaishia kwenye mwaka 2080 hivi.
Sasa kuwanyang'anya kienyeji enyeji haiwezekani, lazima iwe kisheria.

Kauli ya Kigwangwalla ni kauli ya kupuuzwa tu(japokuwa sote tunajua ni Magufuli mwenyewe huenda labda kamtuma kwenda kusema hayo ili kuleta choko choko).
Ngoja tusubiri, muda utatupa majibu.
Watafukuzwa na hawatafanya lolote Unatetea wakoloni?
 
Kwa maamuzi hayo hata mimi namuunga mkono ila ifanyike hivyo na isiwe maneno tu halafu baada ya miezi kadhaa tunaambiwa hiyo kampuni ya Mwarabu inaendelea tena kwa mkataba hulehule OBC )
Hulehule# uleule
 
Back
Top Bottom