Waziri Kigwangalla awacharukia wanaomsema hajui Kiingereza

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Kigwangalla awacharua wanaomsema hajui kingereza asema sio sifa kuijua

Waziri wa Maliasilia na Utalii, Dk. Hamis Kigwangalla amesema kuna watu huwa wanajaribu kumkosoa lugha yake ya kingereza.

“Huwa nina washangaa sana maana kwanza siyo sifa kujua lugha hiyo mimi naitumia kama njia ya kuwasiliana tu,” aliandika Kigwangalla katika ukurasa wake wa Twitter.

Aliongezea kuwa “Ningekuwa sijui kiswahili ama kikimbu na mtu akanicheka angekuwa na mantiki.

1591587748496.png

Waziri anaihifadhi lugha ya Kiingereza kuwasiliana na watalii na katika masuala ya kikazi tu. Hapendi ujinga.
 
Naunga mkono hoja,kutojua lugha fulani hakuondoi usomi wa mtu,,ila kwa nchi yetu ukijua kiingereza tu basi utatazamwa kwa jicho tofauti

Humu ndani kuna "nyani" bingwa wa kiingereza hatari,ukibahatika kujua kiingereza kama cha yule kwa nchi yetu wewe ni msomi hata kama ni la saba
 
Chuo gani hicho? Mheshimiwa inaelekea anaabudu msosi 😂
Sky Eclat pitia hapa

Tulikuwa na tabia ya kupika wali kwenye ‘rice cooker’. Aliyekuwa Mrajis Msaidizi wakati huo alipiga marufuku, kwa sababu za kiusalama. Hatukuacha. Tulijificha zaidi.

Siku moja akafanya ukaguzi wa kushtukiza. Dogo alikuwa anapika. Mimi sipo. Watu wakakimbia wakaambizana. Dogo naye akapata taarifa. Akatorosha vyombo na misosi yote kwa dirishani, baada ya kufunga mlango kwa ndani na yeye akatoroka. Sijui alitorokaje. Ilikuwa floor ya kwanza!

Harufu ya wali iliyojaa chumbani ilisaliti. Profesa alikagua chumba hadi chumba huku akinusa harufu. Akabaini ni chumbani kwangu. Alikijua fika maana kilikuwa cha Rais mstaafu. Akafungua kwa ‘Master Key’ yake. Hakukuta mtu. Akaweka ‘lock’ ili nikirudi nikaripoti ndipo nifunguliwe.

Nikaarifiwa nikawahi maana la sivyo dogo angepata shida pa kulala. Mimi nilikuwa nishaoa na nimepanga Msasani. Kipindi hicho nilikuwa mwaka wa tano. Nililala chumbani pale mara chache tu nilipokuwa najisomea usiku wodini pamoja na wenzangu.

Nilipomfuata Prof., aling’aka kwa hasira, kwa kuwa hakuwa na ushahidi, na kwa kisirani, akanirudishia funguo zangu huku akiapa kunikomesha! Alianza kunitafuta darasani. ‘Akanikamata!’ #NjeYaBox #HK
 
Mimi kipindi kiingereza kipo sheki nilibahatika kukutana na Natives wenyewe,Americans. Waligundua kiingereza si lugha yangu hivyo wakawa wananiongelesha kwa spidi ndogo ili nielewe na mimi nikawa najibu kwa uwezo wangu na nikawa naeleweka.Ila kuna Mkenya fulani tulikuwa naye yeye alikifahamu sana tu na akawa anaona atapata ujiko zaidi kwa udhaifu wangu.Ila chakushangaza kazi nyingi zikawa zinakuja kwangu.
Siku moja nikawauliza mabosi wetu kulikoni,mbona mimi napata kazi nyingi kuliko yule jamaa.Wakasema wamependa jinsi ninavyofanya kazi zangu.Nikawauliza kuhusu lugha yangu sababu mwenzangu accent yake ilikuwa nearly American.Wakasema hilo nisijali,kwa spirit niliyonayo ntajua tu.Mwisho wakaniambia wanaenjoy kusikia Foreign Accent.
Baadaye kikakaa kichwani,japo si kivile.Sasa WaTz wenzangu huu ujasiri wa kuchekana kwenye lugha za kigeni sijui tunautoa wapi.
 
Sky Eclat pitia hapa

Tulikuwa na tabia ya kupika wali kwenye ‘rice cooker’. Aliyekuwa Mrajis Msaidizi wakati huo alipiga marufuku, kwa sababu za kiusalama. Hatukuacha. Tulijificha zaidi.

Siku moja akafanya ukaguzi wa kushtukiza. Dogo alikuwa anapika. Mimi sipo. Watu wakakimbia wakaambizana. Dogo naye akapata taarifa. Akatorosha vyombo na misosi yote kwa dirishani, baada ya kufunga mlango kwa ndani na yeye akatoroka. Sijui alitorokaje. Ilikuwa floor ya kwanza!

Harufu ya wali iliyojaa chumbani ilisaliti. Profesa alikagua chumba hadi chumba huku akinusa harufu. Akabaini ni chumbani kwangu. Alikijua fika maana kilikuwa cha Rais mstaafu. Akafungua kwa ‘Master Key’ yake. Hakukuta mtu. Akaweka ‘lock’ ili nikirudi nikaripoti ndipo nifunguliwe.

Nikaarifiwa nikawahi maana la sivyo dogo angepata shida pa kulala. Mimi nilikuwa nishaoa na nimepanga Msasani. Kipindi hicho nilikuwa mwaka wa tano. Nililala chumbani pale mara chache tu nilipokuwa najisomea usiku wodini pamoja na wenzangu.

Nilipomfuata Prof., aling’aka kwa hasira, kwa kuwa hakuwa na ushahidi, na kwa kisirani, akanirudishia funguo zangu huku akiapa kunikomesha! Alianza kunitafuta darasani. ‘Akanikamata!’ #NjeYaBox #HK
Wakati wenu mambo yalishaanza kukorogeka mpaka mnajipikia. Au ndiyo mlikuwa mnapenda vinono...😂😂?
 
😂😂😂😂ndo maana sitaki kabisa kuhama Tanzani.. tzraha
 
Kigwangalla awacharua wanaomsema hajui kingereza asema sio sifa kuijua

Waziri wa Maliasilia na Utalii, Dk. Hamis Kigwangalla amesema kuna watu huwa wanajaribu kumkosoa lugha yake ya kingereza.

“Huwa nina washangaa sana maana kwanza siyo sifa kujua lugha hiyo mimi naitumia kama njia ya kuwasiliana tu,” aliandika Kigwangalla katika ukurasa wake wa Twitter.

Aliongezea kuwa “Ningekuwa sijui kiswahili ana kikimbu na mtu akanicheka angekuwa na mantiki.

View attachment 1471687

Waziri anaihifadhi lugha ya Kiingereza kuwasiliana na watalii na katika massala ya kikazi tu. Hapendi ujinga.
Asione aibu kwenda kwa Ras Simba
 
Back
Top Bottom