Waziri Kikwete: PSSSF imeanza kulipa mafao kwa kikokotoo kipya kilichoboreshwa

Waziri Kikwete: PSSSF imeanza kulipa mafao kwa kikokotoo kipya kilichoboreshwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), umeanza kutekeleza maagizo ya serikali ya kuanza kulipa Mafao kwa kutumia utaratibu wa Kikomkotoo kilichoboreshwa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete ametangaza.

Kikwete ametangaza hayo leo Novemba 20, 2024 jijini Dar es Salaam, mbele ya Wastaafu watarajiwa wanaochangia PSSSF wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wa namna bora ya kuishi baada ya ksutaafu.
WhatsApp Image 2024-11-20 at 17.29.06_cec2d452.jpg

Ridhiwani Kikwete akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Abdul-Razaq Badru wakati wa kuhitimisha semina za wastaafu watarajiwa wa PSSSF.
WhatsApp Image 2024-11-20 at 17.29.35_2a5f31a2.jpg

Wastaafu watarajiwa wa PSSSF, akifatilia hotuba ya Ridhiwani Kikwete akiwa atahitimisha Semina za wastaafu watarajiwa wa PSSSF.

“Serikali ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ilisikia kilio cha wastaafu, na leo hii ninapenda kutangaza rasmi kwamba hadi kufikia jana (Novemba 19, 2024), jumla ya wastaafu elfu 10,414 ambao wamestaafu kuanzia Julai 2022 na kuanza kulipwa kwa kutumia kikokotoo kile kilicholeta taharuki wameshalipwa mapunjo na kazi bado inaendelea.”

Amesema Kikwete na kuongeza..Lakini jumla ya wastaafu wapya elfu 2,479 ambao wamestaafu kuanzia Julai 1, 2024 wameshalipwa mafao yao kwa kutumia kikokotoo kipya kilichoboreshwa na kazi bado inaendelea,” amesisitiza.

Aidha, serikali imeridhia maboresho yafuatayo yafanyike kuanzia mwezi Januari 2025, ambayo ni pamoja na Wsataafu ambao wengi wamekuwa wakipokea kile kima cha chini cha kiasi cha shilingi 100,000.00, sasa kuanzia pensheni ya Januari 2025 pensheni yao ya mwezi itaongezeka kutoka shilingi 100,000 hadi shilingi 150,000.00.

Na Wastaafu ambao walikua wakipokea pensheni ambayo ni zaidi ya 150,000.00 na wao watapewa ongezeka la asilimia 2 kila mmoja, ameongeza.

Katika maboresho hayo, pia mstaafu yoyote anayepokea pensheni katika Mfuko wa PSSSF akifariki, Mfuko utatoa kiasi cha shilingi 500,000.00 kwaajili ya maziko (funeral grant), huku Mstaafu yoyote akifariki wategemezi wake wanaotambulika na sheria ya Mfuko watalipwa mkupuo wa miezi 36 wa pensheni ya mwezi ya mstaafu husika.

“Utaratibu huu ulishaanza tangu Julai 2022 lakini ulikuwa unatumika kwa wastaafu waliokuwa wanalipwa kwa kikokotoo kipya, lakini sasa utaratibu huu unafunguliwa kwa wastaafu wote hadi wale waliolipwa kwakutumia vikokotoo vya zamani vya kwenye mifuko iliyounganishwa.” Amefafanua Mhe. Kikwete.

Aidha, Kikwete amewahakikishia wastaafu kuwa ustahamilivu wa Mfukoa PSSSF umeendelea kuimarika kutoka asilimia 22 hadi kufikia asilimia 36.4 hivi sasa.

Akimkaribisha Kikwete kutoa hotuba yaek, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Abdul-Razaq Badru, amesema, tangu kuanzishwa kwa Mfuko wa PSSSF tayari umelipa jumla ya mafao yenye kiasi cha shilingi trilioni 10.46 kwa wanufaika 310,458.

“Kwa kiasi hiki kilicholipwa ndani ya miaka sita ya Mfuko, kinaonesha haja ya kuandaa mpango wa mafunzo maalumu kwa ajili ya Wanachama wake wanaotarajia kustaafu ndani ya kipindi cha miaka miwili; Mafunzo haya yatalenga maeneo ya uwekezaji katika viwanda vidogo vidogo na vya kati, uwekezaji katika masoko ya fedha, kilimo biashara na ujasiriamali kwa ujumla."
 
Ahahahahh 🤣 🤣 🤣 🤣
Usimwamini mwana CCM.
Wanachofanya ni kubadili jina tu from kikokotoo kipya to kikokotoo kipya kilichoboreshwa
Hata kile kipya walikipigia promo sana
 
My Take,Mama Hana baya na jasho la mtu.

1. Amewalipa waliopunjwa na sheria ya kikokotoo

2. Amewalipa waliokuwa wamenyimwa hela zao za Wafanyakazi hewa

3. Amewalipa Vifuta jasho wote ambao walivunjiwa Makazi Kwa visingizio vya wako ndani ya Barabara

4. Amewalioa fidia watu wa Jangwani.

5. Anawahamisha masaia Kwa kuwalipa pesa,kuwajengea Makazi na kuwapa Ardhi.

Hongera Samia Kwa moyo wa huruma.

Ila Bado haujawarekebishia watu wa Fao la Kujitoa hasa Kwa Privately Sector au wasio na Ajira za Kudumu, inaumiza sana.

===============

AS of yesterday up to 10,414 retirees who left service starting from July 2022 and received benefits calculated using the old formula, have been reimbursed the due amounts based on the new formula.

Ridhiwani Kikwete, the Labour, Youth, Employment and Persons with Disabilities state minister in the Prime Minister's Office (PMO), disclosed this at a seminar for prospective retirees of the Public Service Social Security Fund (PSSSF) in Dar es Salaam yesterday.

Additionally, 2,479 new retirees as of July 1, 2024 have already received their benefits under the updated calculation formula, with the process ongoing as directed by President Samia Suluhu Hassan.

The government had addressed retirees' concerns by introducing improvements in the 2024/25 budget allocations, including updating the benefits calculation formula, he said

The Guardian
 
PSSSF hii bora kikoba. Fao la uzazi mtu anamaliza miezi miwili hapewi hela. Wanufaika wengine wakidai hela zao ni ngonjeratu
 
Back
Top Bottom