Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,278
- 797
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Thabit Kombo (Mb.) ameagana na Rais wa Bunge la Cuba Mhe. Esteban Hernandez baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi nchini.
Akiwa nchini kwa ziara ya kikazi Mhe. Hernandezi alikutana na kuzungumza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluh Hassan, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi.
Mhe. Hernandez pia alitembelea Kiwanda cha viwatilifu hai cha Biotech Product Limited (TBPL) kilichopo Kibaha mkoani Pwani.
Tanzania na Cuba ni marafiki wa muda mrefu, ambapo urafiki wao uliasisiwa na waliokuwa Viongozi wa Mataifa hayo Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Rais wa kwanza wa Cuba Fidel Castro.
Msingi huu imara wa kihistoria unaendelea kukuza na kuendeleza uhusiano kati ya Tanzania na Cuba kupitia sekta za afya, elimu, na diplomasia.