Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,773
- 1,174
Waziri Kombo akutana na benchi la ufundi la MKICC
Mapema leo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo amekutana na benchi la ufundi (technical team) linalosimamia ujenzi wa kituo kipya cha kimataifa cha mikutano cha ‘Mount Kilimanjaro International Convention Centre’ (MKICC).
Kikao hicho kimefanyika sambamba na uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) na Baraza la Uongozi la Kituo cha Uhusiao wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim.
Kikao kilijumuisha wadau kutoka AICC na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kikilenga kupitia hatua za utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa MKICC. Kituo hicho cha kisasa zaidi, kinatarajia kuwa na ukumbi mkubwa wa mikutano wenye uwezo wa kuchukua watu takribani 5,000, hoteli za nyota tano, na maduka makubwa ya bidhaa (shopping malls).

Attachments
-
IMG-20250606-WA0044.jpg384.5 KB · Views: 27 -
IMG-20250606-WA0062.jpg389.6 KB · Views: 31 -
IMG-20250606-WA0043.jpg345.8 KB · Views: 31 -
IMG-20250606-WA0061.jpg523.1 KB · Views: 28 -
IMG-20250606-WA0057.jpg353.9 KB · Views: 30 -
IMG-20250606-WA0054.jpg368.9 KB · Views: 32 -
IMG-20250606-WA0056.jpg453.9 KB · Views: 28 -
IMG-20250606-WA0059.jpg574.7 KB · Views: 28