Waziri Kombo akutana na Meya wa Mji wa Dallas

Waziri Kombo akutana na Meya wa Mji wa Dallas

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,773
Reaction score
1,174
Waziri Kombo akutana na Meya wa Mji wa Dallas

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo ya heshima na Meya wa jiji la Dallas Marekani, Mhe. Eric Johnson, katika Ofisi ndogo za Wizara, jijini Dar Es Salaam.

Akizungumza baada ya kumkaribisha, Waziri Kombo alimshukuru Mhe. Johnson kwa ziara yake Wizarani na amehaidi kumpa ushirikiano wote utaohitajika ili kumwezesha kutekeleza mkakati wake wa kujenga mtandao wa shughuli za kiuchumi kati ya Wafanyabiashara wa Dallas, Marekani na Tanzania kupitia majukwaa ya kibiashara, uwekezaji na Biashara za Kimataifa.

Naye Mhe. Johnson amesema lengo la kukutana na Mhe. Kombo ni kujitambulisha rasmi pamoja na kuimarisha uelewa wake kuhusu majukumu na vipaumbele vya Wizara, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kukuza ushirikiano kati ya Tanzania na Wadau wa Kimataifa.

Bwana Johnson ambaye ni mara ya kwanza kutembelea Afrika ikiwemo Tanzania; yuko nchini kwa ziara ya siku tatu iliyoanza tarehe 21 Julai, 2025 ili kujifunza kuhusu Tanzania na fursa za kiuchumi zilizopo ambazo zitasaidia kujenga uhusiano wa moja kwa moja wa Uwekezaji na Biashara na Wananchi wa Dallas katika sekta mbalimbali.

“Ninayo furaha kubwa kutembelea Afrika na hasa Tanzania, ni nchi nzuri sana, yenye utajiri mkubwa ikiwemo maliasili; wananchi wakarimu; wanaopenda kujenga uhusiano kwa kutumia fursa za nchi yao na kujiunganisha katika mitandao ya dunia ya kiuchumi na kibiashara ili kujiletea maendeleo” Alifafanua Mhe. Johnson

Mhe. Johnson aliambatana na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Dkt. Elsie Kanza, pamoja na viongozi wa jiji la Dallas akiwemo Mkuu wa Utawala Bi. Alheli Garza, Mkuu wa Itifaki na Uhusiano wa Kimataifa Bi. Beth Huddleston, pamoja na Meneja wa Masuala ya Kimataifa, kutoka Ofisi ya Masuala ya Kiserikali na Ushirikiano wa Kistratejia ya jiji hilo la Dallas.

Mkutano huo uliratibiwa Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Uchumi na Biashara ya Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushrikiano wa Afrika Mashariki Balozi John Ulanga.

FB_IMG_1753342192936.jpg
FB_IMG_1753342262945.jpg
IMG-20250724-WA0161.jpg
IMG-20250724-WA0153.jpg
FB_IMG_1753342198025.jpg
 

Attachments

  • FB_IMG_1753342260738.jpg
    FB_IMG_1753342260738.jpg
    199.6 KB · Views: 23
  • FB_IMG_1753342265446.jpg
    FB_IMG_1753342265446.jpg
    140.5 KB · Views: 28
waziri anakutana na meya aisee yani uwaziri wake ni useless kwa nchi kubwa kule kukutana waziri mwenzake
 
waziri anakutana na meya aisee yani uwaziri wake ni useless kwa nchi kubwa kule kukutana waziri mwenzake
Najua minyumbu yote ya chadema imechanganyikiwa maana Kila wanavyojaribu kumharibia mama ndo kwanza anazidi kung'aa na kustawi, lakini linyumbu hili limepitiliza......yaani limedoda kabisaaa.
 
Back
Top Bottom