Waziri Kombo akutana na Mgombea wa Qatar nafasi ya Mkurugenzi wa WHO

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
651
Reaction score
433
π—ͺπ—”π—­π—œπ—₯π—œ π—žπ—’π— π—•π—’ π—”π—žπ—¨π—§π—”π—‘π—” 𝗑𝗔 π— π—šπ—’π— π—•π—˜π—” π—ͺ𝗔 𝗀𝗔𝗧𝗔π—₯ π—žπ—”π—§π—œπ—žπ—” π—‘π—”π—™π—”π—¦π—œ 𝗬𝗔 π— π—žπ—¨π—₯π—¨π—šπ—˜π—‘π—­π—œ π— π—žπ—¨π—¨ π—ͺ𝗔 π—ͺ𝗛𝗒

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo (Mb.)amekutana na Mshauri wa Waziri Mkuu wa Qatar anayesimamia Masuala ya Afya ya Umma na ambaye ni mgombea wa Serikali ya Qatar katika nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Hanan Mohamed pembezoni mwa Kikao cha 81 cha Baraza kuu ka Umoja wa Mataifa jijini Newyork Marekani.

Katika mazungumzo hayo, viongozi hao wamejadili namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Qatar, hususan katika sekta ya afya, pamoja na kubadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali ya afya na maendeleo katika ngazi ya kimataifa.

Waziri Kombo ameipongeza Serikali ya Qatar kwa nafasi yake muhimu katika kuchangia maendeleo ya kimataifa, pamoja na ushiriki wake wa muda mrefu katika kuunga mkono ajenda za afya na maendeleo duniani.

Aidha, Waziri Kombo amewasilisha ujumbe wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akisisitiza dhamira ya Tanzania ya kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, hususan katika sekta ya afya, ikiwa ni muhimu ya juhudi za kuboresha ustawi wa wananchi na kujenga Taifa lenye afya na maendeleo endelevu.

Kwa upande wake, Dkt. Al Kuwari amewasilisha dira na vipaumbele vyake kwa WHO, na kubadilishana mawazo na Waziri Kombo kuhusu namna ya kukabiliana na changamoto za afya duniani, kuimarisha mifumo ya afya, pamoja na kuongeza uwezo wa nchi katika kukabiliana na dharura za kiafya.
 
Attachments

  • IMG-20261002-WA0002.jpg
    IMG-20261002-WA0002.jpg
    108.1 KB · Views: 9
  • IMG-20261002-WA0001.jpg
    IMG-20261002-WA0001.jpg
    119.3 KB · Views: 11
  • IMG-20261002-WA0000.jpg
    IMG-20261002-WA0000.jpg
    105.6 KB · Views: 7
π—ͺπ—”π—­π—œπ—₯π—œ π—žπ—’π— π—•π—’ π—”π—žπ—¨π—§π—”π—‘π—” 𝗑𝗔 π— π—šπ—’π— π—•π—˜π—” π—ͺ𝗔 𝗀𝗔𝗧𝗔π—₯ π—žπ—”π—§π—œπ—žπ—” π—‘π—”π—™π—”π—¦π—œ 𝗬𝗔 π— π—žπ—¨π—₯π—¨π—šπ—˜π—‘π—­π—œ π— π—žπ—¨π—¨ π—ͺ𝗔 π—ͺ𝗛𝗒

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo (Mb.)amekutana na Mshauri wa Waziri Mkuu wa Qatar anayesimamia Masuala ya Afya ya Umma na ambaye ni mgombea wa Serikali ya Qatar katika nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Hanan Mohamed pembezoni mwa Kikao cha 81 cha Baraza kuu ka Umoja wa Mataifa jijini Newyork Marekani.

Katika mazungumzo hayo, viongozi hao wamejadili namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Qatar, hususan katika sekta ya afya, pamoja na kubadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali ya afya na maendeleo katika ngazi ya kimataifa.

Waziri Kombo ameipongeza Serikali ya Qatar kwa nafasi yake muhimu katika kuchangia maendeleo ya kimataifa, pamoja na ushiriki wake wa muda mrefu katika kuunga mkono ajenda za afya na maendeleo duniani.

Aidha, Waziri Kombo amewasilisha ujumbe wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akisisitiza dhamira ya Tanzania ya kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, hususan katika sekta ya afya, ikiwa ni muhimu ya juhudi za kuboresha ustawi wa wananchi na kujenga Taifa lenye afya na maendeleo endelevu.

Kwa upande wake, Dkt. Al Kuwari amewasilisha dira na vipaumbele vyake kwa WHO, na kubadilishana mawazo na Waziri Kombo kuhusu namna ya kukabiliana na changamoto za afya duniani, kuimarisha mifumo ya afya, pamoja na kuongeza uwezo wa nchi katika kukabiliana na dharura za kiafya.
kila la kheri Dkt. Hanan Mohamed :NoGodNo:
 
Back
Top Bottom