Waziri Kombo akutana na Mwakilishi wa UNFPA nchini

Waziri Kombo akutana na Mwakilishi wa UNFPA nchini

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
publer-1741090895277.jpg

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) amekutana na kuzungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu (UNFPA), Bw. Mark Schreiner katika ofisi za Wizara jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo yao Mhe. Waziri Kombo ameishukuru UNFPA kwa ushirikiano mzuri inaoutoa kwa Serikali katika utoaji wa elimu ya uzazi kwa mabinti walioko shule ili kupunguza mimba na ndoa za utotoni, kuimarisha afya ya mama na mtoto na kutokomeza ukeketaji.

publer-1741090884292.jpg

Mhe. Waziri pia ameipongeza UNFPA kwa matumizi mazuri ya takwimu katika uchambuzi wa utekelezaji wa malengo ya kitaifa na ya Maendeleo Endelevu (SDGs) yatakayofikia kilele mwaka 2030.

Waziri Kombo pia ameiambia UNFPA kuwa ni muhimu kwao kuwatambua wakunga wa jadi ambao wamekuwa wakitumika maeneo ya vijijini kutoa huduma ya kwanza na hivyo kuwa na mafunzo maalum kwao ili kuokoa maisha ya mama na watoto wanaopita mikononi mwao badala ya kupuuza uwepo wao katika jamii.

publer-1741090890712.jpg

Kwa upande wake Bw. Schreiner ameipongeza Tanzania kwa kupunguza idadi ya vifo vya akina mama na watoto, ambapo vifo vya wajawazito vimeshuka kutoka 556 kwa kila vizazi hai 100,000 mwaka 2020 hadi kufikia vifo 104 kwa kila vizazi hai 100,000 mwaka 2024 huku vifo vya watoto chini ya miaka mitano vikipungua kutoka 67 kwa kila vizazi hai 1,000 mwaka 2020 hadi 43 mwaka 2024.

Alieleza kuwa jitihada hizo zimeiongezea sifa na heshima Tanzania katika ulingo wa Kimataifa na hivyo kuisukuma Taasisi ya Gates Foundation kumtunuku tuzo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Bw. Schreiner ameongeza kuwa UNFPA mbali na elimu ya afya ya uzazi imejidhatiti kuwaongezea mabinti wadogo elimu ya ujasiriamali ili waweze kujitegemea na kujiinua kiuchumi.

UNFPA ni miongoni mwa taasisi za Umoja wa Mataifa zenye mchango mkubwa kwa nchi, ambapo Serikali imeazimia kudumisha ushirikiano nao katika kipindi kijacho
 

Attachments

  • publer-1741090897287.jpg
    publer-1741090897287.jpg
    70.2 KB · Views: 1
  • publer-1741090899199.jpg
    publer-1741090899199.jpg
    66.9 KB · Views: 1
  • publer-1741090888906.jpg
    publer-1741090888906.jpg
    88 KB · Views: 1
  • publer-1741090892534.jpg
    publer-1741090892534.jpg
    74.4 KB · Views: 1
  • publer-1741090886432.jpg
    publer-1741090886432.jpg
    77.5 KB · Views: 1
Back
Top Bottom