Waziri Kombo aongoza kikao cha wizara mbili za Tanzania na Balozi wa China

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,773
Reaction score
1,174
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Kombo (Mb.) amefanya kikao kazi na Balozi wa China nchini, Mhe. Chen Mingjian pamoja na Wizara ya Ujenzi na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam leo tarehe 6 Desemba 2025.

Mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha ushirikiano katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na kampuni za China ikiwemo miradi ya ujenzi wa barabara, majengo pamoja na viwanja vya michezo na kubaini maeneo mapya ya ushirikiano kwa siku za mbeleni.

Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Kombo ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa ushirikiano wake katika kuimarisha diplomasia ya uchumi na Tanzania kupitia miradi ya maendeleo katika sekta za ujenzi, ikiwemo ujenzi wa Barabara za Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) katika mkoa wa Dar es Salaam na ujenzi wa majengo ya Serikali jijini Dodoma.

Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi, Mhe. Abdallah Ulega ameishukuru China kwa mchango wake katika kutekeleza miradi ya ujenzi nchini, na kusisitiza umuhimu wa kampuni za ujenzi kukamilisha miradi ya maendeleo kwa wakati ili kuruhusu utekelezaji wa miradi mipya ijayo, katika muda uliopangwa.

Naye Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma ameipongeza China kwa kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na Tanzania, huku akisisitiza umuhimu wa mataifa hayo mawili kupanua wigo wa ushirikiano kwa manufaa ya wananchi wao na vizazi vijavyo.

Awali, Balozi wa China nchini, Mhe. Chen Mingjian, amepongeza juhudi za Serikali ya Tanzania katika kuwezesha utoaji wa fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo, jambo lililochangia kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo na kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa.

IMG-20251206-WA0119.jpg
IMG-20251206-WA0130.jpg
IMG-20251206-WA0128.jpg
IMG-20251206-WA0165.jpg
 
Hizi habari za upande mmoja hizi 🚮🚮upande wa pili unapewa para ya mwisho kama background ama supportive wakati ndiyo upande mkuu 😮‍💨😮‍💨 juzi alipokutana na Balozi za ulaya iliandikwa hivi jioni yake Balozi zile zikatoa taarifa tofauti
 
The Chinese know that you are at your weakest hence they are going to take full advantage of your weak position!! Tutaona Wachina wanawaletea mikataba kede kede mtie saini kuwauzia mali zetu kwa bei ya Chee nyie mafedhuli!!
The Vultures are Patient Birds
 
𝗪𝗮𝘇𝗶𝗿𝗶 𝗞𝗼𝗺𝗯𝗼 𝗮𝗼𝗻𝗴𝗼𝘇𝗮 𝗸𝗶𝗸𝗮𝗼 𝗰𝗵𝗮 𝘄𝗶𝘇𝗮𝗿𝗮 𝗺𝗯𝗶𝗹𝗶 𝘇𝗮 𝗧𝗮𝗻𝘇𝗮𝗻𝗶𝗮 𝗻𝗮 𝗕𝗮𝗹𝗼𝘇𝗶 𝘄𝗮 𝗖𝗵𝗶𝗻𝗮

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Kombo (Mb.) amefanya kikao kazi na Balozi wa China nchini, Mhe. Chen Mingjian pamoja na Wizara ya Ujenzi na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam leo tarehe 6 Desemba 2025.

Mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha ushirikiano katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na kampuni za China ikiwemo miradi ya ujenzi wa barabara, majengo pamoja na viwanja vya michezo na kubaini maeneo mapya ya ushirikiano kwa siku za mbeleni.

Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Kombo ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa ushirikiano wake katika kuimarisha diplomasia ya uchumi na Tanzania kupitia miradi ya maendeleo katika sekta za ujenzi, ikiwemo ujenzi wa Barabara za Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) katika mkoa wa Dar es Salaam na ujenzi wa majengo ya Serikali jijini Dodoma.

Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi, Mhe. Abdallah Ulega ameishukuru China kwa mchango wake katika kutekeleza miradi ya ujenzi nchini, na kusisitiza umuhimu wa kampuni za ujenzi kukamilisha miradi ya maendeleo kwa wakati ili kuruhusu utekelezaji wa miradi mipya ijayo, katika muda uliopangwa.

Naye Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma ameipongeza China kwa kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na Tanzania, huku akisisitiza umuhimu wa mataifa hayo mawili kupanua wigo wa ushirikiano kwa manufaa ya wananchi wao na vizazi vijavyo.

Awali, Balozi wa China nchini, Mhe. Chen Mingjian, amepongeza juhudi za Serikali ya Tanzania katika kuwezesha utoaji wa fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo, jambo lililochangia kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo na kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa.

View attachment 3512466View attachment 3512467View attachment 3512468View attachment 3512475
Mwewe kaona mzoga
 
Hizi habari za upande mmoja hizi 🚮🚮upande wa pili unapewa para ya mwisho kama background ama supportive wakati ndiyo upande mkuu 😮‍💨😮‍💨 juzi alipokutana na Balozi za ulaya iliandikwa hivi jioni yake Balozi zile zikatoa taarifa tofauti
Wachina hawana hayo mambo.
 
Back
Top Bottom