Waziri Kombo apokea nakala za Hati za utambulisho kutoka kwa Mabalozi wateule wa Zimbabwe, Italia na Rwanda nchini

Waziri Kombo apokea nakala za Hati za utambulisho kutoka kwa Mabalozi wateule wa Zimbabwe, Italia na Rwanda nchini

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
Waziri Kombo apokea nakala za Hati za utambulisho kutoka kwa Mabalozi wateule wa Zimbabwe, Italia na Rwanda nchini
454202444_1025614449194725_8584460882700435196_n.jpg
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thatib Kombo (Mb.) amepokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Zimbabwe nchini, Mhe. Helen Bawange Ndingani, Balozi Mteule wa Italia nchini, Giuseppe Sean Coppola na Balozi Mteule wa Rwanda nchini, Mhe. Jenerali Patrick Nyamvumba katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaaam tarehe 5 Agosti, 2024.

Akipokea nakala hizo Waziri Kombo amewapongeza mabalozi hao kwa uteuzi waliuopata na pia amewaahidi ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yao kwa kipindi watakachokuwa nchini kuziwakilisha nchi zao.

Aidha, ameeleza Mabalozi hao Wateule wanatarajiwa kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 12 na 13 Agosti, 2024.

454293838_2275064162845746_4706483941747047587_n.jpg
454122854_1402633903750325_3670713481214388494_n.jpg
 

Attachments

  • 454337849_849912673375694_4817638093940931191_n (1).jpg
    454337849_849912673375694_4817638093940931191_n (1).jpg
    116.4 KB · Views: 5
Back
Top Bottom