Waziri Kombo Apokea rasmi nakala ya Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Kenya nchini Tanzania

Waziri Kombo Apokea rasmi nakala ya Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Kenya nchini Tanzania

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
651
Reaction score
433
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), amepokea rasmi nakala ya Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Jamhuri ya Kenya nchini Tanzania, Mhe. Catherine Karemu, Machi 3, 2026.

Mhe. Kombo amempongeza Balozi Karemu kwa uteuzi wake na kueleza kuwa Wizara itaendelea kushirikiana kwa karibu na Ubalozi wa Kenya katika kipindi chake cha uwakilishi. Vilevile, amesisitiza umuhimu wa kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo.

Katika mazungumzo yao, viongozi hao wamejadili maeneo mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya, ikiwemo jitihada za kuondoa vikwazo vya kibiashara (NTBs) ili kurahisisha biashara kati ya raia wa nchi hizo jirani. Aidha, wameangazia hatua za kuongeza thamani ya mazao ya biashara ndani ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa manufaa ya uchumi wa kikanda.

Mazungumzo hayo pia yamegusia maandalizi yanayoendelea ya Kikao cha Wakuu wa Nchi wa EAC kinachotarajiwa kufanyika Machi 7, jijini Arusha.
IMG-20260303-WA0084.jpg
IMG-20260303-WA0076.jpg
IMG-20260303-WA0082.jpg
IMG-20260303-WA0075.jpg
IMG-20260303-WA0082.jpg
 

Attachments

  • IMG-20260303-WA0081.jpg
    IMG-20260303-WA0081.jpg
    545.1 KB · Views: 22
  • IMG-20260303-WA0078.jpg
    IMG-20260303-WA0078.jpg
    532.8 KB · Views: 24
  • IMG-20260303-WA0085.jpg
    IMG-20260303-WA0085.jpg
    504.3 KB · Views: 19
  • IMG-20260303-WA0080.jpg
    IMG-20260303-WA0080.jpg
    382.8 KB · Views: 29
  • IMG-20260303-WA0073.jpg
    IMG-20260303-WA0073.jpg
    422.5 KB · Views: 23
  • IMG-20260303-WA0071.jpg
    IMG-20260303-WA0071.jpg
    324.1 KB · Views: 21
Back
Top Bottom