Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,773
- 1,174
Waziri Kombo ashiriki Maadhimisho ya Miaka 35 ya Uhuru wa Namibia, Atoa Wito wa Umoja kwa Maendeleo ya Afrika
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) ameshiriki katika Maadhimisho ya Miaka 35 ya Uhuru wa Namibia, ambapo ametoa wito kwa nchi za Afrika kuimarisha Umoja katika kuleta Maendeleo na kutatua changamoto zinazojitokeza Barani Afrika.
Hafla ya maadhimisho hayo ilifanyika tarehe 31 Julai, 2025 katika hoteli ya katika hoteli ya Golden Tulip, jijini Dar Es Salaam.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Kombo amesema Umoja wa Afrika ndio silaha kuu ya kukabiliana na changamoto za sasa kama umasikini, njaa, madeni na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi.
Ameipongeza Namibia kwa mafanikio makubwa iliyopata tangu ilipopata uhuru wake tarehe 21 Machi 1990, kwani imepiga hatua ya kujivunia katika ukuaji uchumi, ujenzi wa miundombinu bora na ukuaji wa maendeleo ya jamii.
“Zawadi kuu na labda ya thamani zaidi ambayo mtu anaweza kuipata ni uhuru—uhuru dhidi ya uonevu, unyonyaji na ubaguzi. Kwa hakika, thamani ya zawadi hii inazidi zawadi zote na hata rasilimali za asili duniani. Ndugu zetu wa Namibia walipata zawadi hii miaka 35 iliyopita, na kwa sababu hiyo, leo tuna kila sababu ya kusherehekea,” alifafanua Mhe. Waziri Kombo.
Aidha, Waziri alikumbusha urafiki wa kihistoria kati ya Tanzania na Namibia, akieleza jinsi nchi hizo zilivyoshirikiana wakati wa harakati za ukombozi wa Afrika.
“Tanzania inajivunia kuwa sehemu ya historia ya uhuru wa Namibia. Hayati Sam Nujoma aliwahi kuwa na hati ya kusafiria ya Kitanzania, akifahamika kama Sam Mwakangale, katika harakati za kupigania uhuru wa nchi hiyo” alibainisha Mhe. Kombo.
Waziri Kombo pia alitumia fursa hiyo kumpongeza Balozi wa Namibia nchini anayemaliza muda wake Mheshimiwa Lebbius Tangeni, kwani amekuwa Rafiki wa kweli wa Tanzania na mshirika wa karibu ambaye amechangia vyema katika kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.