Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,773
- 1,174
Waziri Kombo Ashiriki Maadhimisho ya Siku ya Taifa ya Canada. Apongeza Ushirikiano wa Maendeleo kati ya Tanzania na Canada
Katika kuadhimisha Siku ya Canada, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeipongeza na kuishukuru Serikali ya Canada na Wananchi wake, kwa kukuza ushirikiano wa maendeleo na Tanzania, na hivyo kuimarisha uhusiano wa kihistoria, kiuchumi, na kijamii kati ya mataifa haya mawili.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Mahmoud Thabit Kombo ametoa salaam kwenye hafla ya maadhimisho ya Siku ya Canada iliyofanyika tarehe 1 Julai,2025 katika Makazi ya Balozi wa Canada, jijini Dar es Salaam.
Waziri Kombo amesema Tanzania inajivunia uhusiano wake wa muda mrefu na wa kirafiki na Canada, ambao umechangia kuleta maendeleo ya Taifa kupitia sekta mbalimbali.
“Miradi inayofadhiliwa na Canada kama ‘Her Market, Our Planet’, AHADI na ACELI Africa ni mifano ya ushirikiano kati ya Canada na Tanzania ambayo inachochea maendeleo jumuishi na endelevu. Miradi hii inawawezesha vijana na wanawake kiuchumi na hivyo kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuendeleza kilimo jumuishi,” alibainisha Mhe. Waziri Kombo.
Mhe. Kombo pia ameipongeza Canada kwa kufanikisha uchaguzi wake mkuu uliofanyika tarehe 28 Aprili, 2025 kwa amani na uwazi, akitaja tukio hilo kama ushahidi wa dhamira ya taifa hilo kuendeshwa imara na katika misingi ya demokrasia na utawala wa sheria.
“Tunapata msukumo kutoka Canada tunapojiandaa na uchaguzi wetu mkuu. Tumejifunza kutoka kwa marafiki zetu,” Mhe. Kombo alieleza.
Naye Balozi wa Canada nchini Mhe. Emily Burns, ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano mzuri uliopo kati ya nchi hizi mbili na ameahidi kuimarisha ushirikiano huo kwa manufaa ya vizazi vijavyo na kwa ajili ya maendeleo endelevu ya taifa.