Waziri Kombo atembelea maonesho ya kimataifa ya biashara ya Cuba

Waziri Kombo atembelea maonesho ya kimataifa ya biashara ya Cuba

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
mini_magick20241106-12549-7gws15.jpg

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo tarehe 05 Novemba, 2024 ametembelea Maonesho ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea jijini Havana.

Maonesho hayo yamewakutanisha wafanyabiashara wa ndani na Kimataifa ambao wanatangaza huduma na bidhaa zao ili kuongeza wateja, kukuza soko, kuboresha huduma pamoja na kupeana uzoefu na wafanya biashara wengine.

mini_magick20241106-12549-6ckav4.jpg

Miongoni mwa mabanda aliyoyatembelea Waziri Kombo ni pamoja na banda la Kampuni ya LABIOFARM iliyowekeza nchini kwa kujenga kiwanda cha viuadudu kwa ajili ya kudhibiti malaria kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) kilichopo Kibaha, Pwani.

Kampuni hiyo pia kupitia miundombinu iliyopo ina uwezo wa kuzalisha mbolea na viwatilifu hivyo, itasaidia kuondoa changamoto katika shughuli za kilimo na kuongeza ajira kwa watanzania na wacuba.

mini_magick20241106-12549-18yk86.jpg

Mabanda mengine ni pamoja na kampuni ya Kimataifa ya Havana Club ambayo inazalisha na kuuza vinywaji mbalimbali ikiwemo mvinyo na vinywaji vikali. Tayari kampuni hiyo imeonesha nia ya kuongeza mauzo yake nchini Tanzania na kupata wasambazaji zaidi.
 

Attachments

  • mini_magick20241106-12549-pylkjy.jpg
    mini_magick20241106-12549-pylkjy.jpg
    90.9 KB · Views: 3
  • mini_magick20241106-12549-9w378t.jpg
    mini_magick20241106-12549-9w378t.jpg
    119.5 KB · Views: 3
  • mini_magick20241106-12549-dj4aks.jpg
    mini_magick20241106-12549-dj4aks.jpg
    83.2 KB · Views: 3
  • mini_magick20241106-12549-w9ui9c.jpg
    mini_magick20241106-12549-w9ui9c.jpg
    132.7 KB · Views: 4
  • mini_magick20241106-12549-jwradq.jpg
    mini_magick20241106-12549-jwradq.jpg
    93.5 KB · Views: 4
  • mini_magick20241106-12549-nw3cpv.jpg
    mini_magick20241106-12549-nw3cpv.jpg
    97.9 KB · Views: 3
  • mini_magick20241106-12549-cvjcx8.jpg
    mini_magick20241106-12549-cvjcx8.jpg
    131.9 KB · Views: 3
Wametujengea shule, hospitali, viwanda, wameshiriki katika vita vya ukombozi Angola na Afrika Kusini
Lakini wakipatwa na baa la kimbunga au njaa siye tunajifanya hatuwajui
Fidel Castro alifariki siye hatukuwajua
Kule kwao kuna barabara inaitwa J K Nyerere Road, siye hatuna Castro Rd
Ndo economic diplomacy hiyo!🙁🙁🙁🙁
AIBU !!!!
 
Wametujengea shule, hospitali, viwanda, wameshiriki katika vita vya ukombozi Angola na Afrika Kusini
Lakini wakipatwa na baa la kimbunga au njaa siye tunajifanya hatuwajui
Fidel Castro alifariki siye hatukuwajua
Kule kwao kuna barabara inaitwa J K Nyerere Road, siye hatuna Castro Rd
Ndo economic diplomacy hiyo!🙁🙁🙁🙁
AIBU !!!!
Unataka tumtambue rafiki Fedel Alejandro castro Ruz kwa barabara au namna ya kumuenzi? Kama ni kumuenzi Tanzania Zanzibar ipo secondary school. Peruzi kidogo kabla ya kutuhumu.🙏🙏🙏
 
Back
Top Bottom