Waziri Kombo awasilisha taarifa ya Wizara katika Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU)

Waziri Kombo awasilisha taarifa ya Wizara katika Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU)

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,773
Reaction score
1,174
WAZIRI KOMBO AWASILISHA TAARIFA YA WIZARA KATIKA KAMATI YA NUU

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), ameongoza Menejimenti ya Wizara katika kikao na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU), kilichofanyika jijini Dodoma kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayohusu utendaji wa Wizara na hali ya ushirikiano wa kidiplomasia wa Tanzania.

Katika kikao hicho, Mhe. Kombo aliwasilisha taarifa kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara, ikiwa ni pamoja na hali ya ushirikiano wa Tanzania na jumuiya za kikanda kama vile Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Aidha, Mhe. Kombo aliwasilisha hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa maazimio ya Bunge yanayohusu sekta ya mambo ya nje na diplomasia ya uchumi.

Waziri Kombo pia alieleza mafanikio ya Serikali katika utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje ambayo ni pamoja na kuimarika kwa uhusiano wa kimataifa, hususan kuongezeka kwa ushawishi wa Tanzania katika masuala ya kidiplomasia na hatua zinazochukuliwa kushughulikia changamoto zinazoikabili Wizara.

Kwa upande wake, Kamati ya Bunge iliipongeza Wizara kwa kazi nzuri na kuishauri Wizara kuchukua hatua za makusudi kufanya maboresho zaidi ili Tanzania iweze kunufaika kikamilifu na ushirikiano wa kikanda na kimataifa.

Katika kikao hicho, Mhe. Kombo aliambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi, pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara hiyo, Balozi Samwel Shelukindo na Balozi Stephen Mbundi.
 

Attachments

  • IMG-20250403-WA0040.jpg
    IMG-20250403-WA0040.jpg
    204.3 KB · Views: 36
  • IMG-20250403-WA0035.jpg
    IMG-20250403-WA0035.jpg
    192.3 KB · Views: 38
  • IMG-20250403-WA0032.jpg
    IMG-20250403-WA0032.jpg
    128.2 KB · Views: 31
  • IMG-20250403-WA0033.jpg
    IMG-20250403-WA0033.jpg
    203.1 KB · Views: 40
  • IMG-20250403-WA0031.jpg
    IMG-20250403-WA0031.jpg
    234.7 KB · Views: 24
  • IMG-20250403-WA0037.jpg
    IMG-20250403-WA0037.jpg
    186.5 KB · Views: 30
  • IMG-20250403-WA0041.jpg
    IMG-20250403-WA0041.jpg
    197.8 KB · Views: 35
  • IMG-20250403-WA0039.jpg
    IMG-20250403-WA0039.jpg
    220 KB · Views: 33
  • IMG-20250403-WA0038.jpg
    IMG-20250403-WA0038.jpg
    228.5 KB · Views: 33
  • IMG-20250403-WA0030.jpg
    IMG-20250403-WA0030.jpg
    179.6 KB · Views: 32
  • IMG-20250403-WA0034.jpg
    IMG-20250403-WA0034.jpg
    155.9 KB · Views: 32
  • IMG-20250403-WA0036.jpg
    IMG-20250403-WA0036.jpg
    247.6 KB · Views: 42
  • IMG-20250403-WA0029.jpg
    IMG-20250403-WA0029.jpg
    198.1 KB · Views: 30
Bila shaka hakusemea azimio la bunge la Ulaya na IDU.
 
Back
Top Bottom