Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,278
- 797
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) ataongoza ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Kawaida wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje (RIMC) wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) utakaofanyika jijini Luanda, Angola tarehe 24 Novemba 2024.
Mkutano huo unalenga kupokea na kujadili kuhusu hali ya kisiasa na usalama katika eneo la ukanda wa Maziwa Makuu hususan katika nchi za Jamhuri ya Sudani, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Hatua hiyo inafauatia matukio mbalimbali yaliyotokea katika kipindi cha miongo kadhaa iliyopita kwenye ukanda wa Maziwa Makuu ambayo yamechangia kuzorota kwa hali ya amani na usalama ikiwemo mauaji ya halaiki, ukosefu wa utulivu wa kisiasa, kuwepo kwa mipaka isiyo dhibitiwa, uharifu wa kibinandamu na mivutano ya kugombea madaraka na maliasili.
Hivyo mkutano huo una mchango mkubwa katika kurejesha amani na usalama kwenye ukanda huo kutokana na nafasi yake ya kupendekeza na kusimamia utekelezaji wa mipango na mikakati mbalimbali inayolenga kutatua changamoto hizo ikiwemo mazungumzo, jeshi na kuimarisha utawala bora ili kuchagiza maendeleo ya kiuchumi, kijamii na ushirikiano wa kikanda.
Kadhalika, mkutano huo utapitia na kujadili kuhusu ufanisi wa mipango kazi mbalimbali iliyoandaliwa kwa lengo la kushughulikia migogoro mikubwa katika maeneo mbalimbali kwenye ukanda kiwemo Jamhuri ya Sudani, DRC na Jamhuri ya Afrika ya Kati ili kurejesha na kuimarisha amani na usalama katika maeneo hayo.
Waziri Kombo amewasili jijini Luanda, Angola leo tarehe 22 Novemba 2024 na kupokelewa na Balozi Felisberto Martins Mkurugenzi wa Idara ya America katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Angola, Balozi wa Tanzania nchini humo Mhe. Lt. Gen. Mathew Edward Mkingule mwenye makazi yake nchini Zambia na Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini humo Bw. Mbwana Mziray
PIA SOMA
- Waziri Kombo asisitiza amani na usalama katika Kanda ya SADC