Habari za Zanzibar
JF-Expert Member
- Dec 18, 2024
- 651
- 433
Naomba ifungwe bao nyingi sana na hao wanasiasa huko lolote baya liwakute, mkipata hata goli moja mtasema ni goli la Samuya.𝗪𝗔𝗭𝗜𝗥𝗜 𝗞𝗢𝗠𝗕𝗢 𝗡𝗔 𝗣𝗥𝗢𝗙. 𝗞𝗔𝗕𝗨𝗗𝗜 𝗪𝗔𝗜𝗧𝗘𝗠𝗕𝗘𝗟𝗘𝗔 𝗞𝗔𝗠𝗕𝗜 𝗬𝗔 𝗧𝗔𝗜𝗙𝗔 𝗦𝗧𝗔𝗥𝗦 𝗠𝗜𝗦𝗥𝗜 𝗡𝗔 𝗞𝗨𝗪𝗔𝗞𝗔𝗕𝗜𝗗𝗛𝗜 𝗕𝗘𝗡𝗗𝗘𝗥𝗔 𝗬𝗔 𝗧𝗔𝗜𝗙𝗔.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, wameitembelea Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” iliyokita kambi jijini Cairo nchini Misri.
View attachment 3517125
Waziri Kombo na Profesa Kabudi, wameitembelea kambi hiyo Desemba 17, 2025 na kuikabidhi bendera ya Taifa, ikiwa ni ishara ya kuitakia kila la kheri na kuitia shime kuelekea kwenye kinyang’anyiro cha michuano ya Kombe la AFCON huko nchini Morocco kinachotarajiwa kuanza kutimua vumbi mwishoni mwa mwaka huu.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Balozi Kombo amewasihi vijana hao wachache kati ya wengi wa taifa hili kwa kutanguliza uzalendo kwanza na kuipigania bendera ya Taifa kwa jasho na damu ili kuliletea heshima taifa la Tanzania.
View attachment 3517121
Kwa upande wake, Mhe. Prof. Kabudi, amekiahidi kikosi hicho ushirikiano wa kila aina katika kuhakikisha kikosi hicho kinafanya vyema katika michuano hiyo mikubwa na yenye heshima kubwa sio tu barani Afrika bali duniani kwa ujumla.
Aidha, Prof. Kabudi amewahimiza Watanzania kuipenda na kuipa moyo timu yao ya Stars kwa kuwashangilia na wale watakao kuwa na nafasi kwenda kujiunga nao kwenye mechi zao zote watakazocheza huko nchini Morocco.
View attachment 3517129
Ikumbukwe kwamba kikosi cha Taifa Stars kipo kundi C lenye timu za Nigeria, Tunisia na Morocco na kikosi hicho kitaanza michuano hiyo kwa kucheza na moja ya timu bora barani Afrika timu ya Taifa ya Nigeria.
View attachment 3517127View attachment 3517131
Hiyo ndio Dua ya kila mtu yaaniNaomba ifungwe bao nyingi sana hata ikiwezekana wachezaji wavunjike miguu na hao wanasiasa huko lolote baya liwakute, use*nge wenu mkipata hata goli moja mtasema ni goli la Samuya.
Una huruma sana!Ninaomba kwa Mungu kila mechi tupigwe goli 5
Nimecheka mpaka watu wananishangaaWashatia Gundu
🚮Kombo amewasihi vijana hao wachache kati ya wengi wa taifa hili kwa kutanguliza uzalendo kwanza na kuipigania bendera ya Taifa kwa jasho na damu ili kuliletea heshima taifa la Tanzania.
Hivi Kwanini CCM wanapenda kuwapatia vyeo Wazee yani hata Sehemu ya Vijana na Watoto utakuta kiongozi wao ana Mzee kabisa yani, Kwanini tusijifunze kwa Wenzetu Wazungu, Kwanini Waziri wa Michezo na Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Michezo hizi nafasi walitakiwa wapewe Vijana chini ya Miaka 45. CHakushangazi wapo wazee.Wanatapakanya fedha kwa matumizi ya kijinga na kuwabebesha mzigo walavumbi kwa kuongeza matozo kama yote...yaani tunatumia mamilioni kuwasafirisha majizi ili yaende kupeleka bendera?
Kabudi ilitakiwa awe anaelea wajukuu zake lakini bado tu yupo anapambana.Hivi Kwanini CCM wanapenda kuwapatia vyeo Wazee yani hata Sehemu ya Vijana na Watoto utakuta kiongozi wao ana Mzee kabisa yani, Kwanini tusijifunze kwa Wenzetu Wazungu, Kwanini Waziri wa Michezo na Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Michezo hizi nafasi walitakiwa wapewe Vijana chini ya Miaka 45. CHakushangazi wapo wazee.
Kumbuka hao unawaombea wavunjwe miguu ni watanzania na wana ndugu humu,unadhani ni sawa kuwaombea wavunjwe miguu? unadhani ndugu wa hao wachezaji watakupenda? vipi kama ndugu zako ndio wangekuwa wanachezea taifa stars ungwaombea wavunjwe miguu? acha roho mbaya,utakufa vibayaNaomba ifungwe bao nyingi sana hata ikiwezekana wachezaji wavunjike miguu na hao wanasiasa huko lolote baya liwakute, use*nge wenu mkipata hata goli moja mtasema ni goli la Samuya.
Hao wako in partnership na wauaji wa ndugu zetu, secondly wakishinda watataka kumpa sifa muuaji mkuu wa Watanganyika so literally they're one and the same. Wavunjike hata shingo.Kumbuka hao unawaombea wavunjwe miguu ni watanzania na wana ndugu humu,unadhani ni sawa kuwaombea wavunjwe miguu? unadhani ndugu wa hao wachezaji watakupenda? vipi kama ndugu zako ndio wangekuwa wanachezea taifa stars ungwaombea wavunjwe miguu? acha roho mbaya,utakufa vibaya
pole sana kwa mawazo ya hovyo kama hayoHao wako in partnership na wauaji wa ndugu zetu, secondly wakishinda watataka kumpa sifa muuaji mkuu wa Watanganyika so literally they're one and the same. Wavunjike hata shingo.