Waziri Kombo na Prof. Kabudi waitembelea kambi ya taifa stars Misri na kuwakabidhi bendera ya taifa

𝗪𝗔𝗭𝗜𝗥𝗜 𝗞𝗢𝗠𝗕𝗢 𝗡𝗔 𝗣𝗥𝗢𝗙. 𝗞𝗔𝗕𝗨𝗗𝗜 𝗪𝗔𝗜𝗧𝗘𝗠𝗕𝗘𝗟𝗘𝗔 𝗞𝗔𝗠𝗕𝗜 𝗬𝗔 𝗧𝗔𝗜𝗙𝗔 𝗦𝗧𝗔𝗥𝗦 𝗠𝗜𝗦𝗥𝗜 𝗡𝗔 𝗞𝗨𝗪𝗔𝗞𝗔𝗕𝗜𝗗𝗛𝗜 𝗕𝗘𝗡𝗗𝗘𝗥𝗔 𝗬𝗔 𝗧𝗔𝗜𝗙𝗔.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, wameitembelea Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” iliyokita kambi jijini Cairo nchini Misri.

Waziri Kombo na Profesa Kabudi, wameitembelea kambi hiyo Desemba 17, 2025 na kuikabidhi bendera ya Taifa, ikiwa ni ishara ya kuitakia kila la kheri na kuitia shime kuelekea kwenye kinyang’anyiro cha michuano ya Kombe la AFCON huko nchini Morocco kinachotarajiwa kuanza kutimua vumbi mwishoni mwa mwaka huu.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Balozi Kombo amewasihi vijana hao wachache kati ya wengi wa taifa hili kwa kutanguliza uzalendo kwanza na kuipigania bendera ya Taifa kwa jasho na damu ili kuliletea heshima taifa la Tanzania.

Kwa upande wake, Mhe. Prof. Kabudi, amekiahidi kikosi hicho ushirikiano wa kila aina katika kuhakikisha kikosi hicho kinafanya vyema katika michuano hiyo mikubwa na yenye heshima kubwa sio tu barani Afrika bali duniani kwa ujumla.

Aidha, Prof. Kabudi amewahimiza Watanzania kuipenda na kuipa moyo timu yao ya Stars kwa kuwashangilia na wale watakao kuwa na nafasi kwenda kujiunga nao kwenye mechi zao zote watakazocheza huko nchini Morocco.

Ikumbukwe kwamba kikosi cha Taifa Stars kipo kundi C lenye timu za Nigeria, Tunisia na Morocco na kikosi hicho kitaanza michuano hiyo kwa kucheza na moja ya timu bora barani Afrika timu ya Taifa ya Nigeria.

Haituhusu
 
Naomba ifungwe bao nyingi sana hata ikiwezekana wachezaji wavunjike miguu na hao wanasiasa huko lolote baya liwakute, use*nge wenu mkipata hata goli moja mtasema ni goli la Samuya.
Hawa mbona iko wazi watarudisha kende zao hapa baada tu ya mechi tatu za makundi kumalizika.

Timu limekuwa platform ya kujipigia promo za kisiasa na kutafuta popularity kwa watawala wa serikali haramu.

Mpaka hapo tayari imeshatiwa nuksi, na awamu hii hata point moja hawapati.
 
Washaenda kutia nux watu wajue tu Kila sehemu atakapotia miguu mwanasiasa wa ccm basi watanzania wote tutakuwa against na hiyo sehemu. Naomba tufungwe kama netball 8-0
 
𝗪𝗔𝗭𝗜𝗥𝗜 𝗞𝗢𝗠𝗕𝗢 𝗡𝗔 𝗣𝗥𝗢𝗙. 𝗞𝗔𝗕𝗨𝗗𝗜 𝗪𝗔𝗜𝗧𝗘𝗠𝗕𝗘𝗟𝗘𝗔 𝗞𝗔𝗠𝗕𝗜 𝗬𝗔 𝗧𝗔𝗜𝗙𝗔 𝗦𝗧𝗔𝗥𝗦 𝗠𝗜𝗦𝗥𝗜 𝗡𝗔 𝗞𝗨𝗪𝗔𝗞𝗔𝗕𝗜𝗗𝗛𝗜 𝗕𝗘𝗡𝗗𝗘𝗥𝗔 𝗬𝗔 𝗧𝗔𝗜𝗙𝗔.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, wameitembelea Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” iliyokita kambi jijini Cairo nchini Misri.

Waziri Kombo na Profesa Kabudi, wameitembelea kambi hiyo Desemba 17, 2025 na kuikabidhi bendera ya Taifa, ikiwa ni ishara ya kuitakia kila la kheri na kuitia shime kuelekea kwenye kinyang’anyiro cha michuano ya Kombe la AFCON huko nchini Morocco kinachotarajiwa kuanza kutimua vumbi mwishoni mwa mwaka huu.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Balozi Kombo amewasihi vijana hao wachache kati ya wengi wa taifa hili kwa kutanguliza uzalendo kwanza na kuipigania bendera ya Taifa kwa jasho na damu ili kuliletea heshima taifa la Tanzania.

Kwa upande wake, Mhe. Prof. Kabudi, amekiahidi kikosi hicho ushirikiano wa kila aina katika kuhakikisha kikosi hicho kinafanya vyema katika michuano hiyo mikubwa na yenye heshima kubwa sio tu barani Afrika bali duniani kwa ujumla.

Aidha, Prof. Kabudi amewahimiza Watanzania kuipenda na kuipa moyo timu yao ya Stars kwa kuwashangilia na wale watakao kuwa na nafasi kwenda kujiunga nao kwenye mechi zao zote watakazocheza huko nchini Morocco.

Ikumbukwe kwamba kikosi cha Taifa Stars kipo kundi C lenye timu za Nigeria, Tunisia na Morocco na kikosi hicho kitaanza michuano hiyo kwa kucheza na moja ya timu bora barani Afrika timu ya Taifa ya Nigeria.

Na Taifa Star watapokea kuchapo cha mbwa koko. Na wote semeni... Amen
 
Back
Top Bottom