Hivi punde
JF-Expert Member
- Apr 1, 2017
- 2,554
- 8,587
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amesema wizara hiyo haihusiki na kupotea kwa mwandishi wa habari wa kampuni ya Mwananchi Communication Limited (Ltd), Azory Gwanda.
Kangi ametoa kauli hiyo, leo Ijumaa Julai 6, 2018 wakati wa mkutano wake na wanahabari uliofanyika Ofisi ndogo ya wizara hiyo jijini Dar es Salaam.
Waziri huyo ameeleza hayo baada ya kuulizwa swali na mwandishi wa habari aliyetaka kujua mkakati wa Lugola kuhusu kupotea kwa Gwanda tangu Novemba mwaka jana.
Swali: Mheshimiwa waziri hivi karibuni kumekuwa matukio ambayo sisi waandishi wa habari yanatusumbua mojawapo ni kupotea kwa mwanahabari mwenzetu, Gwanda ambaye bado hajaonekana tangu atoweke Novemba mwaka jana.
Polisi wanasema bado hawajachunguza kwa kina. Nini kinachoendelea, hili unalizungumziaje ili waandishi wa habari tufanye kazi katika mazingira salama bila kubughudhiwa.
Lugola: Zipo hizo habari. Mtu yupo nyumbani kwake halafu ametoweka. Sisi mambo ya ndani hatuingilii uhuru wa mtu kutoweka nyumbani kwake. Kila mtu ana uhuru kwa mujibu wa Katiba ya nchi anaweza kutoka sehemu moja kwenda nyingine bila kuvunja sheria.
Waziri Lugola alisema kama Gwanda alitoweka wakati akiwa nyumbani, wao hawahusiki bali wanahusika na mtu aliyetendewa uhalifu ikiwamo kutekwa, akisema katika tukio kama hilo vyombo vya dola humtafuta mtekaji.
“Hawa ambao wanatoweka kwao tu, wanakuwa na sababu nyingi. Kuna wengine maisha yakiwashinda anaamua kwenda kwingine,” alisema.
Lugola alieleza uzoefu wake alipotembelea migodi wakati akiwa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).
"Kwenye migodi nilikutana na watu ambao kwao walishaweka matanga kwa kujua wameshakufa. Kwao hawaonekani, lakini kumbe wametoweka," alisema Lugola
Lugola ameeleza kuwa hicho ndicho anachoweza kusema kwa sasa kuhusu kutoweka kwa Gwanda.
Jeshi la Polisi, ambalo jukumu lake kubwa ni kulinda watu na mali zao, liko chini ya Wiuzara ya Mambo ya Ndani.
PIA, SOMA:
- Mwandishi wa kampuni ya Mwananchi Communications (MCL), Azory Gwanda apotea siku 10 na hajulikani alipo