Waziri Lukuvi apiga marufuku madalali kulipwa posho ya mwezi mmoja na wapangaji. Asema ni ujambazi

Binafsi hadi leo sielewi mantiki ya mwenye kupanga ndiyo amlipe dalali kodi nzima ya mwezi kama ujira na siyo mpangishaji. Bora hata ingekuwa 50/50 kwa mpangaji na mpangishaji.
 
Hizi ni blah blah tu. Hao madalali wa nyumba wanatambulika na Wizara? Atawekaje marufuku kwa vijana wa vijiweni waliojiajiri kama madalali bila vibali? Kwa sheria ipi na mamlaka gani aliyonayo kama Waziri?
 
Tatizo ni matamko ya kisiasa
 
Wafikirie gharama za kutafuta nyumba bila dalali. Ila kodi ya mwezi mzima ni kubwa mno, wangewarasimisha kisha wakaweka viwango.

Mfano Kuonyeshwa nyumba Tsh 10,000/= Ukiipenda unalipa lets say 10% ya kodi na mwenye nyumba anatoa 10% ya kodi.
 
Unadhani mwenye nyumba atakubali nyumba yake ikae bila mpangaji kisa pesa ya dalali?
Sawa amlipe yeye huyo dalali! Sio amtwishe gharama mpangaji huo si uungwana.

Na hata wenye nyumba wanaowalipa madalali hawawapi mwezi mmoja Kama wanavyotaka wapangaji tuchajiwe. Unakuta anapozwa elfu 20 anatulia ila mpangaji anataka ampe mwezi mzima si uhuni huo!
 
Niliwahi kusema hili jambo hapa jamvini, kumbe Lukuvi naye kalisemea
 
Inaumiza ila waweke mfumo mzuri hapo hawasaidii kitu Lasivyo kodi za nyumba zitaongezwa kiholela
 
Wenye nyumba nao sasa ni shida tupu. Unaweza kwenda bila dalali wakakutolea nje.

Ila sijawahi mlipa dalAli pesa ya mwezi. Na ninakoelekea ile elfu 20 wanayochaji itakuwa ndio mwisho wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…