Waziri Lukuvi apiga marufuku madalali kulipwa posho ya mwezi mmoja na wapangaji. Asema ni ujambazi

Huwezi kuzuia madalali kulipwa kwa sababu ni makubaliano rasmi kabla mpangani hajapelekwa kuoneshwa nyumba, kama hutaki basi zoezi linaishia hapo. Hivyo mpangaji atalipa tu atake asitake kama kweli anahitaji nyumba/ chumba.
 
B
Basi madalali ndio wanapandisha Kodi za nyumba ili apate hela nyingi ya mwezi.

Hi serikali balaaa!!!!!!!
 
Wewe kubali nlipe mwenye nyumba dalAli mpe utakachoona. Nawafabyaga hivyo mimi
Ifikie wakati hawa madalali wapokee % ya kodi tu sio kutaka wapewe kodi ya mwezi 100% ni uhuni! Ikibidi utaratibu uwe kama ifuatavyo.

Charges ziwe 20% ya kodi ya mwezi kwa kodi za laki moja au chini ya laki 1!

Kwa kodi za zaidi ya laki 1 charges ziwe 10% ya kodi ya nyumba.

Hai make sense ukalipe kodi ya nyumba 1mil per months kwa miezi 6 ni around 6millions halafu eti dalali umpe million 1 sababu tu kakuonesha nyumba ya kulipia.
 
Kabisa tena ziwe na Rating kabisa .maana kuna nyumba zingine hovyo kabisa.Una weka rating ya maana kuwasanuwa wengine
Kuna kipindi niliwaza kutengeneza huu mfumo na niusajili rasmi uwe unalipa % kama income tax ya serikalini!

Watu wakiuzoea huu ndio inakua kifo cha madalali kama uber na bolt zilivyoua soko la tax za kupelekana mbezi posta kwa 25,000/= 😆😆😆
 
kipindi nasoma second year udsm (2004) miaka hiyo, Zitto kabwe amesababisha mgomo tumetembezewa virungu nikatembea kwa mguu toka hall two hadi kwa kakobe nikikwepa FFU maporini mle, niliamua kwenda kupanga mtaani niachane na hostel, hapo ndipo nilipojua madalali hawana utu, wala huruma na hawaangalii umri.

kuna wababa wawili watu wazima kabisa wakanichukua ati wakanionyeshe chumba, nikamchukua mshikaji wangu mmoja tukaenda nao hadi sinza eneo fulani hivi, wakanionyesha chumba kimoja kichafu na kibaya aisee sijui alikuwa anakaa mbwa, ni kijumbe cha nnje, ghafla wakanambia niwape uchakavu wa kunileta baada ya mimi kushangaa kama kwelii wako serious ndio chumba hicho wamenileta, kumbe muda wote description ya aina ya chumba nilichohitaji waliijua lakini wakaona watapataje uchakavu na mimi ni dogo siwezi kuzingua kuwapa wakinifikisha, nikawapa alfu tano nikaachana nao. ile alfu tano iliniuma hadi leo na sikuelewa kwanini watu wazima wangefanya kitu kama kile. wengine hawa madalali ni matapeli tu.
 
Madalali mshikilie hapohapo wanangu [emoji3577][emoji3][emoji23][emoji23]

Hii nchi bila kuwa "ntu ya dili" hutoboiiii
 
Madalali ni majambazi, unakuta umempa simu akuuzie kwa shilingi 50000 smart phone, yeye anauza laki moja . Sasa dalali yeye anachukua 50,000, na Bado anakudai udalili Kam ten hivi, jumla anakamata kibindoni 60000 ,bila shida anaenda kunywea pombe
 
Huu ujumbe usiishie hapa uchukuliwa kwa mkazo mkali. Madalali ni matapi
 
Hela ya udalali inauma asee, yaani unatoa 70k hivi hivi kwa jamaa anayepiga stori kitaa na umeisotea asee.

Hatukatai madalali wana msaada ila wachukue asilimia flani.
Tena nyumba hajajenga yeye. Kiasi cha kukutembeza kilomita tatu tu basi anakula 70k.

Hakuna pesa inaniuma kama hii ya udalali aisee.
 
Wanaopanga hawana shida kulipa maana si kazi rahisi kupata nyumba.

Sasa kama ni hivo dalali si anaweza kuongea na mwenye nyumba bei iwe juu ,kitu kile kile
Kutokana na kwamba Dalali anaitaka hiyo kodi ya mwenzi mmona Nyumba ya 70k anakaza kwa 100k. Mradi tu anufaike na hiyo ya mwezi mmoja huku anakuumiza wewe miezi 12.

Wamesababisha nyumba kupanda bei. Fremu za biashara ndio usisema. Kisa hiyo ya mwezi.
 
South Africa iwe nyumba au ofisi-Kodi ni Kwa Mwezi moja mmoja+kodi ya mwezi kama deposit(dhamana ya Nyumba au ofisi uliyopangishwa) Siku unarudisha chumba/ofisi mwenye Nyumba anakagua kama umearibu kitu mfano umevunja kioo cha dirisha au koki ya maji bafuni aifungi tena etc-atakata garama ya matengenezo toka kwenye Deposit yako.

Wakati nikiwa huko my best friend alikuwa ni real estate agent(kule unasomea kwanza ndo upewe leseni yake) akipangisha nyumba yeye anaongeza ka profit margin kidogo.Mfano kama nyumba ni laki tatu yeye atacharge 320 to 350(serikali imeweka viwango vinavyotakiwa kisheria) So kila kodi ikilipwa anapata % yake kwa mwezi. so akiwa amepangisha nyumba 100 kwa mfano na anapata 20-50K kwa mwezi anaweza pata mpaka 5M kwa mwezi na kwa mwaka up to 100M .Alikuwa na ofisi nzuri tu na tulikuwa tunaishi powa sana na inakuwa biashara endelevu kwa Dalali(real estate agent) kwani anapata hela kila Mwezi.

Hapa ni risk business kwa madalali-No future kwao! asipoenda kijiweni kwao hapati deal za wapangaji wapya so analala njaa.Akisafiri pia akuna hela kwake...akishapata kodi ya mwezi ndo basi tena kumbe angeweza pata 30K kila mwezi ata kama yupo Amana Hospital kalazwa😁😁. TUKUTANE MKUU TUMWONE LUKUVI TO ESTABLISH STARTUP COMPANY YA HAYA MAVITU. source code nnayo pia DM me please tuyajenge
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…