Waziri Lukuvi atekeleza agizo la Rais Magufuli, aikabidhi Halmashauri ya Kigamboni ekari 715 za ardhi

Waziri Lukuvi atekeleza agizo la Rais Magufuli, aikabidhi Halmashauri ya Kigamboni ekari 715 za ardhi

Hiyo Taarifa Sijaelewa hizo ekari 715 zilikua zinamilikiwa na Quality Group kupitia international Village Ltd

Zimefikaje mikononi Mikononi mwa Halmshauri kupitia Wizara ya Ardhi ??
Quality Group Wamepokonywa ?? Wameuzia Serikali ??
Ufafanuzi Tafadhali
Sheria ya ardhi na 2,soma sambamba na sheria ya vijiji na 5,ni makosa kwa mtu binafsi au taasisi kumilikishwa ZAIDI YA EKARI 50 bila ya kupata kibali cha Rais
Hizo ekari 700 Manji alipewa na wizara kwa kushirikiana na manispaa ya Temeke,hiyo kuifanya ardhi hiyo kuwa ni haramu kisheria
Ardhi ikibainika kuwa ilihalallishwa kiharamu,serikali inawajibu wa kuitwaa na kuigawa upya.
 
Sisi tunasikiliza sauti ya Rais bwashee!
Rais alisemaje kuhusu matumizi ya ardhi hiyo ikirudishwa? Na je Lukuvi kama waziri hajui maelekezo ya rais hadi atoe kauli hiyo kwamba ardhi iliyorudishwa itakuwa ni kwa matumizi ya umma na sio kiwanja au makazi ya mtu mmoja mmoja?
 
... Rais wa JMTZ anayo mamlaka ya ku-revoke umiliki wa ardhi yoyote kutoka kwa yeyote kwa matumizi yeyote yatakayompendeza yeye bila kuhojiwa na yeyote popote wakati wowote ndani ya mipaka ya nchi. Hata kipande cha ardhi unachomiliki wewe (kama unacho) umekasimiwa tu umiliki wake kwa niaba ya Rais na ikimpendeza atakitwaa muda wowote without prior notice.

In short, Rais ndiye custodian wa ardhi yote ya Tanzania.

Without prior notice? You need to go through the following statutes again

The Land Act Cap 113 (R.E 2002)
The Village Land Cap 114 (R.E 2002)
Land Acquisition cap 118 (RE 2002)

You have a fair understanding of acquisition (and land) laws but the issue you talked about hapo juu needs better understanding

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais alisemaje kuhusu matumizi ya ardhi hiyo ikirudishwa? Na je Lukuvi kama waziri hajui maelekezo ya rais hadi atoe kauli hiyo kwamba ardhi iliyorudishwa itakuwa ni kwa matumizi ya umma na sio kiwanja au makazi ya mtu mmoja mmoja?
Maamuzi yote wamepewa halmashauri ya Kigamboni......ikiwemo kuhakikisha wafanyakazi wa wilaya ya Kigamboni wanapatiwa makazi wilayani humo!
 
... Rais wa JMTZ anayo mamlaka ya ku-revoke umiliki wa ardhi yoyote kutoka kwa yeyote kwa matumizi yoyote yatakayompendeza yeye bila kuhojiwa na yeyote popote wakati wowote ndani ya mipaka ya nchi. Hata kipande cha ardhi unachomiliki wewe (kama unacho) umekasimiwa tu umiliki wake kwa niaba ya Rais na ikimpendeza atakitwaa muda wowote without prior notice.

In short, Rais ndiye custodian wa ardhi yote ya Tanzania. Yaani linapokuja suala la umiliki wa ardhi yeye ndiye ALFA na OMEGA.
Hii Sidhani kama ni Sawa
Na kama ni Sawa pengine Kuwe na utaratibu unaofuata baada ya kuki-twaa hicho Kiwanja Chako

Na Kama si hivyo unaterminate Vipi umiliki wa ardhi ya Mtu na ulifuata taratibu zote huoni apo inaleta Sura ya Uonevu ??
 
Maamuzi yote wamepewa halmashauri ya Kigamboni......ikiwemo kuhakikisha wafanyakazi wa wilaya ya Kigamboni wanapatiwa makazi wilayani humo!
... utajiri huo mchana kweupe kwa watumishi idara ya ardhi Kigamboni. Sitashangaa badala ya kupimwa vizuri yakaibuka makazi holela mithili ya Manzese hapo.
 
Hii Sidhani kama ni Sawa
Na kama ni Sawa pengine Kuwe na utaratibu unaofuata baada ya kuki-twaa hicho Kiwanja Chako

Na Kama si hivyo unaterminate Vipi umiliki wa ardhi ya Mtu na ulifuata taratibu zote huoni apo inaleta Sura ya Uonevu ??
... kwa kuwa marais wetu nao ni binadamu wana feelings na utu ndio maana hawawezi kufanya unyama wa kiwango hicho. Ila akitokea "mwendawazimu" sheria zetu zimempa mamlaka hayo.
 
Sheria ya ardhi na 2,soma sambamba na sheria ya vijiji na 5,ni makosa kwa mtubaubtaasisi kumilikishwa ZAIDI YA EKARI 50 bila ya kupata kibali cha Rais
.

Hivi hizo Sheria ni Mpya Ama?
Ina Maana Quality Group,Wizara na Manispaa wote walihusiku kufanya hiy biashara Haramu ??

Anyway hiyo Sheria sikuwa naifahamu thanks for let me know
 
Without prior notice? You need to go through the following statutes again

The Land Act Cap 113 (R.E 2002)
The Village Land Cap 114 (R.E 2002)
Land Acquisition cap 118 (RE 2002)

You have a fair understanding of acquisition (and land) laws but the issue you talked about hapo juu needs better understanding

Sent using Jamii Forums mobile app
Kasome sheria namba 2 sambamba na namba 5 ya kijiji
Ni kosa kwa mtu au taasisi kumilikishwa zaidi ya ekari 50,bila ya kupatabkibali cha Rais
Huyo Manji alimwaga mpunga akaishia wizarani akapewa ardhi enzi hizo
Kisheria,chochote halali kilichopatikana haramu kinageuka kuwa haramu,without prior notice!
 
Je,Kikwete hakutoa kibali?Kama hakutoa,waliohusika kutoa ardhi hiyo bila kibali cha Rais wamechukuliwa hatua gani?
 
thanks for let me know
= Thanks for letting me know!
Usije ukauziwa pori ekari 100 ukapewa hati utanyang'anywa tu
Kijiji au halmashauri kuuza/kupima/kumilikisha mwisho ekari 50,zikizidi faili lazima liende kwa mwenye ardhi tuliompa atutunzie ardhi yetu
Kamishna wa ardhi ataonesha kwa nini anataka kugawa ardhi yote hiyo,je kuna maslahi yoyote yatapatikana kwa hilo kabaila likipewa neema hizo za Mungu,je wananchi watanufaika vipi,Rais akiridhika atatoa go ahead
Tanzania tuna sheria nzuri/ngumu sana za ardhi,ndio mana wakenya wameishiwa nguvu katika kupigania EAC
 
Je,Kikwete hakutoa kibali?Kama hakutoa,waliohusika kutoa ardhi hiyo bila kibali cha Rais wamechukuliwa hatua gani?
Wahusika wameshastaafu,mpaka juzi Rais kateua kamishna mwingine,na umeona remarks zake wakati wa kumuapisha
Halafu hilo ni eneo moja tu,kuna mabomu huko ardhi unaweza kulia
Sofia Simba kamilikishwa pwani yote ya kusini mashariki kuanzia Gomvu kwenda kusini karibu kilometa 50 za beach,zote zake
Serikali inakosa mapato,kila anaetaka kuweka hoteli akiweka GPS akienda wizarani anaambiwa pana mtu!
 
Back
Top Bottom