Mtumishiwetu
Senior Member
- Jul 13, 2022
- 196
- 346
Huenda uteuzi wa Waziri wa Ardhi, Angelina Mabula ukatenguliwa wakati wowote kuanzia sasa kwa kile kinachodaiwa kuwepo kwa mgongano wa kimaslahi kutokana na uamuzi wake wa kusitisha utoaji wa vibali vya ujenzi wa vituo vya mafuta.
Uamuzi huo umetangazwa leo Alhamisi Novemba 10, 2022 na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula.
“Lengo ni kutoa nafasi kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na wizara zinazohusika na utoaji wa vibali kufanya tathmini ya kina kuhusu ujenzi wa vituo vya mafuta nchini,” amesema.
Aidha, Dk Angeline ameagiza kusitishwa kutolewa kwa vibali vipya vya ujenzi vinavyokiuka mipango kabambe ya majiji, manispaa, miji na kusitisha ugawaji wa viwanja kiholela unaosababisha taswira za miji kuharibika.
Habari zaidi zinasema maamuzi hayo yatawagusa watoto wa wakubwa ambao wanadaiwa kwa sehemu kubwa wanajishughulisha na biashara ya mafuta