BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Baadhi ya vigogo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliogombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Jumuiya ya Wazazi, wamebwagwa akiwamo aliyekuwa Mwenyekiti Dk. Edmund Mndolwa.
Vigogo wengine walioshindwa ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk. Angelina Mabula, na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima, waliogombea nafasi ya wajumbe watatu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).
Akitangaza matokeo hayo jana jijini Dodoma, Msimamizi wa Uchaguzi huo, Maalim Kombo Hassan, alimtangaza Fadhil Maganya aliyeshinda kwa kura 578 akimwacha mbali Dk. Mndolwa aliyepata kura 64.
Katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Doto Iddi Mabrouk alitangazwa kuwa mshindi kwa kupata kura 530 kati ya 736 zilizopigwa akiwashinda wagombea wengine wanne.