Waziri Makamba: Hakuna uhaba wa mafuta nchini, amtaka Mkurugenzi wa TPDC akajieleze kabla hawajachukua hatua

Ona jinga hili
 
Makamba anadhani nchi hii yuko peke yake. Ukweli ni huo uliosemwa na Mataragio. Pamoja na bei kuwa juu, kampuni za mafuta zinapata hasara kwa miezi miwili sasa kutokana na bei elekezi kuwa chini. Jamaa wameiambia Serikali wataagiza mafuta kama watakubali kuwafidia hasara wanayopata kwa sasa.
 
Mimi nadhani alitaka kuweka worse case scenario kwamba ikitokea meli haijafika ila alikosea sababu bulk system ndio wanajukumu hilo kuhakikisha wale walioshinda tender wanaleta kwa wakati na hii imekuwa toka 2012 sasa mkurugenzi wa TPDC hii sio kazi yake kusemea serikali nadhani ameshajuwa kuna chance TPDC wakarudishiwa wao wawe kama waagizaji pekee kitu ambacho hakitatokea wameshanusa ulaji sasa wamefufuka. Kwa kauli hii mkuregenzi wa TPDC kaingilia mamlaka sio yake kabisa maana hata yeye na kampuni yake wameshinda tender kwa kushindana na wengine hawakupewa tu kama zawadi. Waziri yuko sahihi jamaa kachemka ila naamini hakuwa na nia mbaya ila hakuliweka sawa na vile waandishi wetu hawa wanadaka moja baya tu.
 
Hiyo wizara ishamshindwa,siasa za blah blah na uongo mwingi ndio anazoziweza,hiyo wizara mama angemrudisha prof muhongo tu ndio angalau kidogo aliiweza
 
Mimi sioni kosa la mkurugenzi hapo.
Yeye kaeleza kitakachotokea endapo Meli itapata tatizo.

Hilo linawezekana na mfano mzuri ni Zanzibar; walipoanzisha utaratibu kama huo wa serikali kuagizamafuta ili kuwa ikitokea uhaba wa mafuta pale Meli ilipopata hitlafu ama kuchelewa. Walioko Zanzibar ni mashahidi wa hili
 
wafuasi wa Chadema kama kawaida yao na tabia zao za kigaidi za kutaka nchi iwe ktk taharuki na shida,
muda wote wao wanataka habari mbaya ziikumbe Tanzania.
kweli nimeamini wafuasi wa mboe wana chembe chembe za kihalifu.

ukiwafuatilia wafuasi wa mboe utagundua mara zote kunapokuwa na tatizo kama nchi basi huwa wao wana shangilia sana.
hawa watu ni hatari sana, mwaka 2025 hawafai hata kupata kiti kimoja cha ubunge.
 
Huyu makamba kaanza kutengeneza vitisho kwa wataalamu, tukiweka hapa CV yake na ile ya mataragio utaelewa tu ni nani anayeongea jambo lenye mantiki, Nyerere aliharibu sana hii nchi kwa kuwapa nguvu wanasiasa.......mwanasiasa mwenye elimu ya kuunga unga anaweza kukurupuka tu na kuanza kuongea maswala yanayotakiwa kutolewa ufafanuzi na wataalamu.....​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…