All truth23
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 1,215
- 1,401
Dah sasa wanaanza kuwalazimisha watu kusema wasichokiamini!!! Hii ni Haibu SANA WACHA WATU WASEME WENYEWE.Waziri wa Nishati, Januari Makamba amesema kazi inafanyika na dhamira nzuri ipo na anachoomba uelewa na uwepo wa subira pamoja na kutiwa moyo.
"Kazi inafanyika na dhamira nzuri ipo tunachoomba ni uelewa na subira tunaomba kutiwa moyo kama hali imeboreka semeni kwamba Sasa hivi ni bora kuliko ilivyokua mkisema sio tunanyong'onyea sababu tumetumia pesa tumetumia muda kurekebisha hii hali" amesema Makamba
Chanzo TBC