Waziri Makamba: Serikali kuanzisha ofisi maalum ya mradi wa LNG, mazungumzo kukamilika Disemba

Getrude Mollel

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2022
Posts
270
Reaction score
362
Waziri wa Nishati, January Makamba, ametembelea ofisi za Kampuni ya Shell, nchini Uholanzi, na kukutana na kuzungumza na viongozi wakuu wa kampuni hiyo kuhusu masuala mbalimbali yanayohusiana na utekelezaji wa mradi wa LNG nchini.

Katika mazungumzo hayo na Bwana Cederic Cremers, Makamu wa Rais anayeshughulikia miradi ya LNG na Bwana John Crocker, Makamu Rais wa Shell anayehusika na Mahusiano ya Serikali, Waziri Makamba alielezea azma ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha mazungumzo yanakamilika mwezi Disemba mwaka huu na hatua za utekelezaji zinaanza mara baada ya hapo.

Katika mikutano hiyo, Waziri Makamba pia alielezea mpango wa Serikali wa kuanzisha Ofisi Maalum ya Kusimamia Utekelezaji wa Mradi wa LNG (Tanzania LNG Office) mnamo mwezi Novemba mwaka huu kwa lengo la kuratibu, kuharakisha na kurahisisha hatua za utekelezaji wa mradi.

Mradi huo wa kuchakata na kusindika gesi asilia iliyogundulika katika bahari kuu Kusini mwa Tanzania, utaleta nchini uwekezaji wenye thamani ya dola za Kimarekani bilioni 40, unatekelezwa na Makampuni ya Shell ya Uholanzi na Equinor ya Norway na washirika wao.

Waziri Makamba alieleza kwamba mradi huo una manufaa mengi kwa Tanzania na utafungua fursa nyingi kwa wananchi wa Mikoa ya Kusini mwa Tanzania na kuiongezea mapato nchi na kuleta ajira na mapinduzi ya kiuchumi na kijamii nchini.

Kwa upande wa Kampuni ya Shell, Bw. Crocker, aliishukuru Serikali ya Awamu ya 6, inayoongwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapa wawekezaji matumaini na kutoa kipaumbele katika mradi huo na kuwezesha kusainiwa kwa mkataba wa awali. Pia alieleza kuridhishwa kwao kwa hatua ya majadiliano iliyofikiwa katika maandalizi ya utekelezaji wa mradi huo. Bw. Crocker alisisitiza nia yao na ya washirika wao ya kutekeleza mradi.
 
Huu mradi huu kila siku mazungumzo tu
 
Ule wa Bomba la Mafuta ya Uganda liliishia wapi au nalo linapelekwa mpechempeche Kama JK Nyerere Dam!
Nchi ngumu hii!
 
Samia anaonekana kuipenda sana hiyo LNG, sijui alianza lini kuipenda, na hayo mapenzi sijui yalisababishwa na nini.

Inashangaza, mradi wa gharama kubwa kama huo, utakaohitaji kiasi kikubwa cha pesa toka kwa muwekezaji huku serikali ikiwa haina uwezo huo, na hatujui muwekezaji atazirudisha vipi pesa zake anazowekeza hapo, halafu Rais wa nchi na waziri wake kutwa kucha kuupigia debe huo mradi, inafikirisha sana.
 
Mali ni yetu na magoti tunapiga sisi.
 
Tunaenda kunyukwa kisawasawa ! Dadeki waulize Nigeria kule niger delta dahari ya miaka mpaka leo [emoji753]️
 
Porojo corrupted goverment haijawahi kuingia mkataba wa maana kwa manufaa ya nchi yao
 
Mikataba ya kuuza nchi itaisha lini?.Ninyi viongozi acheni kuiuza nchi yetu.mkataba gani wa kwenda kusainiwa huko ubeberuni
 
Back
Top Bottom