Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Ila CCM imejaa viongozi wengi wajinga, badala mtilie mkazo kwenye uadilifu, kukemea uchawa na wizi, rushwa na ufisadi, mnakuja kujitia aibu kwa ujinga kama huu! kwani nani hajui kukosolewa kwenu ni matusi? Kukosolewa kwenu ni uchochezi? Kukosolewa kwenu ni kuleta machafuko?
Yaani kama hamtoshei kwenye nafasi zenu mnataka wanachi tusiseme? Kama kichwani hamna kitu mnataka msiambiwe? Tuwape dhamana sisi halafu mkituibia na kwenda kinyume na katiba tusiseme?
Masauni ungekuwa unatoshea kwenye hiyo nafasi hata kwa robo tu usingeongea haya umeongea leo na kuhamasisha vijana wawe chawa, unatia aibu! Yaani manvuliwa nguo kila siku tena na CCM wenzenu halafu unakuja kulaumu wapinzani na wananchi, na mnaona mnafanya la maana kabisa kuja kutisha wanachi kama hivi?
Siku tutakayowakomboa chawa wote, ndio mtaelewa viongozi wengi CCM ukiwemo na wewe hakuna kitu!
#KataaUozo2025
#KataaMachawa
#KataaWajinga2025
===
"Kweli tumekuwa kimya kusemea mazuri ya Dk. Samia na Dk. Mwinyi, tujitathmini tu katika hilo, kwamba je nafanya hayo? Kwasababu kiukkweli Marais wetu hawa wawili wamefanya mambo mambo makubwa sana katika muda mfupi.
"Na bahati mbaya sana tunatoa nafasi kwa wapinzani kufikisha jitihada hizi, kwanini hamuoni kuna viclip vya kijinga jinga vvinasambaa vya wapinzani? Wanadhihaki viongozi wetu, wanadhihaki serikali.
"Sisemi kwamba lazima na wewe utoe clip ujibu lakini hata ukifanya kazi katika eneo ulipo, kama wewe ni balozi , nyumba zako 10 tafuta namna ya kuweza kufikisha ujumbe, kama ni tawi, tawi lako.
"Lakini niwapongeze sana viongozi wetu hawa, hawajatetereka, na sisi tuwe mfano wa kufuata nyayo zao. Wako watu walioona kwamba kwasababu hakuna ajenda, ilani imetekelezwa kwa kiwango kikubwa kabla hata ya wakati, hawa wapinzani wakaona labda pengine watafanya vitu vitasababisha kuteteresha mshikamano na umoja uliopo.
"Wakatishia wengine kutaka kujitoa sijui katika serikali ya umoja wa kitaifa lakini kwa busara za viongozi wetu hawa, wametulia, wanafanya mambo kwa vitendo, hawajatoka kwenye reli.
"Hayo wanafanya lengo lao si tu kututoa kwenye reli lakini vile vile kutaka tunapoelekea kwenda kutekeleza demokrasia ya kuchagua viongozi tunaowataka katika uchaguzi mkubwa unaotarajia kufanyika mwakani ili twende nchi yetu ikiwa haina amani. Jambo hilo haliwezekani.
"Nataka niwahakikishie, hiyo dhamana nimepewa mimi, mimi ndio Waziri wa Mambo ya Ndani, ninayesimamia mapolisi na vyombo vya usalama, watu watafanya uchaguzi katika nchi hii kwa usalama na amani, na mtu yoyote asijaribu kutaka kucheza na amani ya nchi hii, tutailinda amani na usalama wa nchi hii kwa gharama yoyote."
Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni amesema hayo leo Jumapili, Julai 7, 2024 visiwani Zanzibar, kwenye hafla ya kufungua mafunzo ya uongozi wa Chama Cha Mapinduzi na jumuiya zake.