Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Serikali ya Tanzania imeweka wazi sababu ya kumfukuza nchini Kiongozi na Mchungaji wa Kanisa la Christian Life maarufu ‘Kanisa la Kiboko ya Wachawi’, Dominique Dibwe kwa kukiuka misingi na mafundisho ya Vitabu Vitakatifu sambamba na kutoa wito kwa wahubiri wengine kufuata mafundisho ya Vitabu Vitakatifu na Sheria mbalimbali za nchi zinazosimamia taasisi hizo za kidini huku ikikemea matukio ya mauaji na ulawiti yanayoendelea nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati akifunga makambi yaliyoandaliwa na Kanisa la Waadventista Wasabato Maranatha lililopo Mtaa wa Maji ya Chai, Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha.
Amesema “Tulimuondoa Mchungaji mmoja Nchini kwa kukiuka Sheria za Usajili na mmeshuhudia huko anapokwenda amekuwa akisambaza video akithibitisha mambo aliyokuwa akiyafanya ni kinyume kabisa na Kitabu cha Dini ikiwemo kutapeli watu, kuwatoza watu fedha kinyume cha utaratibu, kuwaaminisha Watu miujiza inaweza kuwafanya wawe matajiri.”