Waziri Masauni awataka wanafunzi kutetea misingi ya Muungano

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,922
Reaction score
3,252
f1c66f79-faa6-4901-a133-e73b3d3b4101.jpg
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amewataka wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu nchini na vijana kuendelea kulinda na kutetea misingi ya Muungano iliyoachwa na Waasisi.

Mhandisi Masauni ameyasema hayo Aprili 06, 2026 Jijini Dar es Salaam wakati akifungua kongamano maalum la kumuenzi aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume.

d45c38e1-19b1-46fb-a9eb-9a3eca2dc43b.jpg
Waziri Masauni amesema mwasisi huyo wa Muungano ameacha alama na historia ya kudumu kwa vizazi vya sasa na vijavyo, juhudi zilizotokana na mchango alioutoa katika kuwaunganisha Watanzania na kupambania maslahi ya wananchi wanyonge.

“Leo hii tunapomuenzi Sheikh Abeid Amani Karume tuna mengi ya kujifunza kutoka kwake kwani tumejionea jinsi alivyojali na kutetea maslahi ya wananchi wanyonge na zaidi ni juhudi zake katika kuasisi Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964,” amesema Mhandisi Masauni.

Aidha, Masauni amemtaja Sheikh Abeid Amani Karume Zanzibar kuwa ni kiongozi imara aliyesimamia maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wananchi wa Zanzibar juhudi ambazo zimendelea kusimamiwa katika awamu mbalimbali za uongozi.

Amesema Sheikh Abeid Amani Karume ataendelea kukumbukwa na Watanzania kutokana na kuibua sera zilizogusa hisia za wananchi walio wengi ikiwemo ugawaji bure wa ardhi, utoaji wa elimu bure, matibabu ya bure na ujenzi wa makazi ya kisasa.

“Sheikh Karume aliishi ndoto ya muda mrefu ya uanamajumui wa kiafrika katika kuunganisha Bara zima la Afrika na kuunda Shirikisho la Afrika kwa vitendo na alifanya mambo mengi muhimu ambayo kamwe hayawezi kusahaulika” amesema Mhandisi Masauni.

Awali akimkaribisha Mgeni rasmi, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi amesema kongamano hilo ni la kwanza kufanyika kwa upande wa Tanzania Bara ambalo linalenga kuhamasisha vijana kutambua mchango wa waasisi wa muungano ikiwemo Sheikh Abeid Amani Karume.

Amesema katika kuchagiza elimu ya Muungano, Ofisi hiyo imeandaa programu ya elimu kwa umma ambayo imekusudia kuelimisha wananchi wa makundi mbalimbali ya kijamii ikiwemo vijana na wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu nchini.

fa87bc19-ad5a-42fd-990e-7a03d27ca98a.jpg

Kongamano hilo la siku moja limeandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) kwa kushirikiana na Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa.
 
Muungano uwe na serikali tatu basi, huu uliopo una changamoto na kasoro nyingi sana.
 
Back
Top Bottom