saidoo25
JF-Expert Member
- Jul 4, 2022
- 624
- 1,456
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki amemjibu Rais Samia Suluhu Hassan kuwa agizo lake la kutaka kufutwa kwa vitalu vya Ranchi za Taifa NARCO vinavyomilikiwa kisheria na wawekezaji mbalimbali nchini amelipima na kwamba linahitaji umakini mkubwa kutekelezwa.
"Mh Rais aliagiza vitalu vilivyoko kwenye ranchi zetu za Narco ikiwezekana vifutwe, sasa jambo hili tumelipima na tukaliona linahitaji umakini mkubwa na kwa hiyo ili kutekeleza jambo hili wizara tumeunda timu ya wataalamu kutoka wizara na taasisi mbalimbali zinazohusika na mambo mbalimbali sasa timu hii tunataka ifanye tathmini ya kina ya utendaji na changamoto zilizoko ndani ya Narco ili tuweze kuishauri sawasawa serikali" amesema Mashimba
CHANZO WASAFI MEDIA: