Waziri Mavunde: Kampuni ya Tembo Nickel Yafanikiwa Kusafisha na Kuzalisha Madini ya Nikeli, Shaba na Kobati Kwenye Kiwanda Kilichopo Kabanga, Ngara.

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

WAZIRI MAVUNDE: TEMBO NICKEL YAFANIKIWA KUSAFISHA NA KUZALISHA MADINI YA NIKELI, SHABA NA KOBATI KWENYE KIWANDA KILICHOPO KABANGA, NGARA, HII NI HABARI NJEMA

Kampuni ya Tembo Nickel ambayo Serikali ya Tanzani ni mbia, imepata mafanikio ya kihistoria - kwa mara ya kwanza!

Tembo Nickel kupitia kampuni yake mama ya Lifezone Metals imeandika historia kwa kuzalisha nikeli, shaba, na kobalt zilizosafishwa kutoka kwenye Mradi wa Kabanga Nickel ulioko Ngara, Kagera.

Hatua hii muhimu imefikiwa wakati wa majaribio yaliyofanywa katika Maabara ya Lifezone ya kisasa ya Simulus, kwa kutumia Teknolojia yao ya ubunifu ya Hydromet.

Mafanikio haya yanaendana kikamilifu na maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuongeza thamani ndani ya nchi.

Uzalishaji huu ni wa mara ya kwanza katika kipindi cha karibu miongo mitano tangu ugunduzi wa madini hayo katika eneo la Kabanga.

Kwa mafanikio haya, Tembo Nickel inaweka msingi imara kwa Kiwanda chake cha Usafishaji Metali Anuai kitakachokuwa Kahama,Mkoani Shinyanga ambacho kitazalisha madini ya ubora wa juu yaliyopatikana kwa kuzingatia uendelevu hapa hapa Tanzania,ambacho tayari ya Madini wameshatoa Leseni husika na hivyo kupelekea kuanza kwa hatua za awali za ujenzi wake.

Hii ni hatua muhimu katika kuifanya nchi yetu kuwa kati ya nchi vinara duniani katika uzalishaji wa nikeli ya Daraja la 1 na madini mengine ya kimkakati.

Tanzania iko tayari kukumbatia uwekezaji wa kuchimba madini wenye uwajibikaji na ubunifu ambao unaweka kipaumbele uongezaji wa thamani ndani ya nchi na maendeleo endelevu.

Shirikiana nasi katika safari ya Tanzania kuelekea katika mustakabali ang’avu na wenye mafanikio zaidi katika sekta ya madini duniani!

Anthony Mavunde
Waziri wa Madini
23.07.2014
 
Attachments

  • WhatsApp Image 2024-07-23 at 19.21.55.jpeg
    WhatsApp Image 2024-07-23 at 19.21.55.jpeg
    149.9 KB · Views: 8
  • WhatsApp Image 2024-07-23 at 19.21.52.jpeg
    WhatsApp Image 2024-07-23 at 19.21.52.jpeg
    101.5 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2024-07-23 at 19.21.54(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-07-23 at 19.21.54(1).jpeg
    151.7 KB · Views: 8
  • WhatsApp Image 2024-07-23 at 19.21.54(2).jpeg
    WhatsApp Image 2024-07-23 at 19.21.54(2).jpeg
    118.5 KB · Views: 8
  • WhatsApp Image 2024-07-23 at 19.21.54.jpeg
    WhatsApp Image 2024-07-23 at 19.21.54.jpeg
    49.3 KB · Views: 9
  • WhatsApp Image 2024-07-23 at 19.21.53(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-07-23 at 19.21.53(1).jpeg
    98.7 KB · Views: 8
  • WhatsApp Image 2024-07-23 at 19.21.53.jpeg
    WhatsApp Image 2024-07-23 at 19.21.53.jpeg
    70.3 KB · Views: 9

WAZIRI MAVUNDE: TEMBO NICKEL YAFANIKIWA KUSAFISHA NA KUZALISHA MADINI YA NIKELI, SHABA NA KOBATI KWENYE KIWANDA KILICHOPO KABANGA, NGARA, HII NI HABARI NJEMA

Kampuni ya Tembo Nickel ambayo Serikali ya Tanzani ni mbia, imepata mafanikio ya kihistoria - kwa mara ya kwanza!

Tembo Nickel kupitia kampuni yake mama ya Lifezone Metals imeandika historia kwa kuzalisha nikeli, shaba, na kobalt zilizosafishwa kutoka kwenye Mradi wa Kabanga Nickel ulioko Ngara, Kagera.

Hatua hii muhimu imefikiwa wakati wa majaribio yaliyofanywa katika Maabara ya Lifezone ya kisasa ya Simulus, kwa kutumia Teknolojia yao ya ubunifu ya Hydromet.

Mafanikio haya yanaendana kikamilifu na maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuongeza thamani ndani ya nchi.

Uzalishaji huu ni wa mara ya kwanza katika kipindi cha karibu miongo mitano tangu ugunduzi wa madini hayo katika eneo la Kabanga.

Kwa mafanikio haya, Tembo Nickel inaweka msingi imara kwa Kiwanda chake cha Usafishaji Metali Anuai kitakachokuwa Kahama,Mkoani Shinyanga ambacho kitazalisha madini ya ubora wa juu yaliyopatikana kwa kuzingatia uendelevu hapa hapa Tanzania,ambacho tayari ya Madini wameshatoa Leseni husika na hivyo kupelekea kuanza kwa hatua za awali za ujenzi wake.

Hii ni hatua muhimu katika kuifanya nchi yetu kuwa kati ya nchi vinara duniani katika uzalishaji wa nikeli ya Daraja la 1 na madini mengine ya kimkakati.

Tanzania iko tayari kukumbatia uwekezaji wa kuchimba madini wenye uwajibikaji na ubunifu ambao unaweka kipaumbele uongezaji wa thamani ndani ya nchi na maendeleo endelevu.

Shirikiana nasi katika safari ya Tanzania kuelekea katika mustakabali ang’avu na wenye mafanikio zaidi katika sekta ya madini duniani!

Anthony Mavunde
Waziri wa Madini
23.07.2014
Good direction. Kudos
 
Back
Top Bottom