Waziri Mchengerwa: Haijawahi kutokea kiongozi wa nchi kupita vijijini kama anavyofanya Rais Samia

Waziri Mchengerwa: Haijawahi kutokea kiongozi wa nchi kupita vijijini kama anavyofanya Rais Samia

Mzee wa Chai

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2022
Posts
684
Reaction score
1,202
Waziri wa OR-TAMISEMI akihojiwa na Clouds Media amesema...

Haijawahi kutokea kiongozi wa juu wa nchi kupita maeneo ya vijijini kama alivyofanya Dkt. Samia Suluhu Hassan hasa kipindi ambacho si cha uchaguzi lazima tuliweke hili hewani.

Maeneo ambayo Mhe. Rais amepita siku ya jana maeneo ya Liwale, yale maeneo wananchi walikuwa wakiwaona viongozi wakati wa uchaguzi baada ya uchaguzi hawaoni kiongozi yoyote lakini leo hii Mhe. Rais amepita maeneo hayo kabla ya uchaguzi kwenda kushuhudia fedha anazozipeleka zinatumika ipasavyo kwa wananchi wake wanyonge na wananchi ambao wao ndio tegemeo lake akilala akiamka anawafikiria Watanzania hawa wakawaida wanyonge ambao wako kwenye hali duni anataka kuwanyanyua kuwaweka katika hali nzuri


----

Kwa hili Waziri Mchengerwa umesema kweli tupu, upewe binti mwingine wa mama

Vijijini wanamkubali sana mama, maendeleo ni makubwa huko kwasababu

1. Hawahitaji umeme wataufanyia nini
2. Hawahitaji maji ya visimani na kwenye vijito yanawatosha
3. Barabara washazoea kutembea na miguu na baiskeli inatosha
4. Kilimo cha jembe na kutegemea mvua ndio silaha yao kubwa watake nini tena
5. Shule sio lazima sana watoti watasomea kwenye miti chini imetosha

Asante sana kwa kuupiga mwingi [emoji119]

20230918_130206.jpg
 
Africa tunaishi nyuma ya muda.

Kuishi nyuma ya muda kunawafaidisha wengine. Ili wazidi kufaidika wanafanya kila liwezekanalo ili wenzao wazidi kuishi nyuma ya muda.
 
Matumizi mabaya ya fedha yanatafutiwa maneno yahalalishwe
 
  • Thanks
Reactions: apk
Kwa mfano tulipoenda kumzika Mzee Mengi ilituwia vigumu kuelewa tumeshafika kijijini

Hivyo siyo kwamba Marais hawajawahi kwenda Vijijini ila inategemea ni Vijiji Vya Mkoa gani

Ni hilo tu mh Mchengerwa

Kwako FaizaFoxy 😂😂🐼
 
Mbona nyerere aliwahi kufika kijijini kwangu ndani kabisa kukagua mashamba ya wanakijiji ya bega kwa bega, maarufu kama begabega na mashamba ya ujamaa? Labda marais waliofuatia baada ya yeye hawakuwahi kutembelea vijiji mpaka wakamaliza muda wao wa urais. Anyway, mama anaupiga mwingi, kongole.
 
kuna mawaziri kiukweli kama hasira za watu zingekuwa zinanyonga bc huyu singepona vijana wanatamani kumpiga mawe kwa kugawa ajira zao!
 
Kwa mfano tulipoenda kumzika Mzee Mengi ilituwia vigumu kuelewa tumeshafika kijijini

Hivyo siyo kwamba Marais hawajawahi kwenda Vijijini ila inategemea ni Vijiji Vya Mkoa gani

Ni hilo tu mh Mchengerwa

Kwako FaizaFoxy 😂😂🐼
Sasa mbona unaandika kama vile kila mtu anafahamu huyo Mchengerwa kasema nini???!!!
 
Back
Top Bottom