Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mohammed Mchengerwa ameeleza kuwa hajapata uthibitisho wa madai kuwa kuna vituo vya Uandikishaji Wapiga Kura nchini vimeandikisha baadhi ya watu (Wanafunzi) ambao hawajakidhi vigezo kikanuni kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo Oktoba 15, Waziri Mchengerwa amewataka viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa nchini kufikisha changamoto zao kwa wasimamizi walioko maeneo yote ya nchi ili ziweze kufanyiwa kazi kwa kufuata sheria na kanuni katika mchakato wa uchaguzi.
"Kumekuwepo na taarifa kwamba yapo maeneo ambapo baadhi ya watu wameandikishwa ambao pengine umri wao mdogo. Ni taarifa ambazo nimezisikia, lakini hatujapata uthibitisho wa taarifa hizi. Nichukue fursa hii kueleza kwamba kanuni zetu za uchaguzi zimetoa maelezo ya kina kuhusu ni nani mwenye haki ya kujiandikisha kupiga kura kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa, kuwa ni miaka 18 au zaidi."
Pia, Soma:
=> Watoto wa shule wamekutwa wakiandikishwa katika daftari la Uchaguzi Serikali za Mitaa Luguruni-Kibamba kinyume cha sheria
=> CHADEMA yajipanga kuzuia watoto kupiga kura Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, wabaini madudu haya
=> Kwanini uandikishaji wa wapiga kura serikali za mitaa unafanyika kwenye makaratsi na siyo kidigitali? Ulinzi wa taarifa unahakikishwaje?
=> CHADEMA Nyasa: Watendaji wa Mitaa na Kata wanasimamia na kuandaa orodha ya wapiga kura kinyume na Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa