Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mohammed Mchengerwa ameeleza kuwa hajapata uthibitisho wa madai kuwa kuna vituo vya Uandikishaji Wapiga Kura nchini vimeandikisha baadhi ya watu (Wanafunzi) ambao hawajakidhi vigezo kikanuni kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo Oktoba 15, Waziri Mchengerwa amewataka viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa nchini kufikisha changamoto zao kwa wasimamizi walioko maeneo yote ya nchi ili ziweze kufanyiwa kazi kwa kufuata sheria na kanuni katika mchakato wa uchaguzi.
"Kumekuwepo na taarifa kwamba yapo maeneo ambapo baadhi ya watu wameandikishwa ambao pengine umri wao mdogo. Ni taarifa ambazo nimezisikia, lakini hatujapata uthibitisho wa taarifa hizi. Nichukue fursa hii kueleza kwamba kanuni zetu za uchaguzi zimetoa maelezo ya kina kuhusu ni nani mwenye haki ya kujiandikisha kupiga kura kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa, kuwa ni miaka 18 au zaidi."

Hivi mwanafunzi wa A ĺevel mwenye miaka 18 au 19 asijiandikishe kisa mwanafunzi?
CHADEMA wameishasense watashindwa kwani wanachama wao wa mitandaoni hawaendi kujiandikisha.
Leo watu wameingia uwanjani kusubiria mechi ya Taifa stars tangu saa saba wanapigwa na jua lakini watu hao hao kusimama nusu saa tu wajiandikishe kupiga kura hawataki.
Ukitathmini walkoingia kuangalia mechi ya leo huenda zaidi ya robo tatu hawajajiandikisha.